Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- NAIBU WAZIRI MAHUNDI AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA
- MRADI WA REGROW KUCHOCHEA UCHUMI WA WANANCHI WANAOPAKANA NA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA.
- DC. MALISA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA
- Wiki ya huduma kwa Mteja, Mbeya UWSA kituo cha kuchotea maji wananchi Soko Matola chazinduliwa
- WASIOJULIKANA WABOMOA SHULE.
- MZRH YAENDELEA KUWA KITUO CHA MFANO KATIKA USIMAMIZI WA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
- SENETI MKOA WA WA MBEYA WAMUOMBA MWENYEKIT KUWASIMAMIA MIKOPO INAYOTOLEWA NA JIJI
- Mbeya UWSA yaadhimisha wiki ya mteja kwa kuwapongeza Mawakala wake
Author: Mbeya Yetu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb), ametaja mambo makubwa aliyoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Sekta ya Maliasili na Utalii. Ameyasema hayo leo Septemba 24, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Peramiho, Mkoani Ruvuma. Mhe. Chana amesema kuwa Rais ameifungua dunia kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kupitia filamu yake ya “Tanzania the Royal Tour “ sambamba na kuielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kufungua Utalii Kusini. Ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania kuitazama filamu hiyo na kutembelea vivutio mbalimbali vya…
UMOJA WA MABUNGE DUNIANI WAJIHAKIKISHIA USHIRIKIANO ENDELEVU NA UMOJA WA MATAIFA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amethibitisha kuwa ushirikiano endelevu baina ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa (UN) ni wa muhimu katika kutekeleza ajenda mbalimbali za pamoja kwa manufaa ya dunia.
Dkt. Tulia alitoa kauli hiyo tarehe 23 Septemba, 2024, alipokuwa akiwasilisha hotuba kwa niaba ya IPU katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliojadili mustakabali wa dunia kwa siku zijazo (Summit of the Future), uliofanyika katika Ofisi za UN jijini New York, Marekani.
Akiwasilisha hotuba yake, Dkt. Tulia alieleza kuwa kwa zaidi ya robo karne tangu kuanzishwa kwa Azimio la Milenia, ushirikiano kati ya IPU na UN umeonesha mafanikio makubwa, ambapo kwa kila mwaka wameweza kufikia malengo ya kuiwezesha UN kuwa Taasisi inayowajibika, yenye uwazi na inayotekeleza maazimio yake ipasavyo.
Aidha, alibainisha kuwa nafasi ya Mabunge imeainishwa wazi katika lengo namba 55 la Azimio la Pact of the Future, ambalo linaelekeza kuimarisha ushirikiano kati ya Mabunge na Umoja wa Mataifa.
Akisisitiza umuhimu wa wajibu wa Mabunge, Dkt. Tulia alinukuu maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyesema “Inawezekana, tekeleza wajibu wako” akiongeza kuwa Umoja wa Mabunge Duniani unatimiza wajibu wake kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa unaendelea kuwa imara kwa kupitia Mabunge.
“Dunia inahitaji mabadiliko na sehemu pekee ya kufanya mabadiliko hayo ni ndani ya Umoja wa Mataifa, na wakati wa kufanya hivyo ni sasa,” alisisitiza Dkt. Tulia.
MHE. MAHUNDI AFUNGUA MKUTANO MKUU WATATU WA UMOJA WA MAAFISA UHUSIANO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyoanza leo Septemba 22 na kumalizika kesho Septemba 23, 2022. Akizungumza na Waandishi hao Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki Dkt Zakia aliwataka kuzingatia mafunzo wanayopewa, dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa weledi. Mafunzo hayo ni…
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya likiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo limefanya mazoezi ya “Show Force” kuzunguka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ikiwa ni sehemu ya doria za kuimarisha ulinzi na usalama.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa upo umuhimu wa mataifa mbalimbali duniani kuboresha na kubadilisha mifumo ya kiutawala na ugawaji bora wa rasilimali ili kuwezesha utekelezaji wa Agenda ya 2030 ya Maendeleo endelevu kwa ufanisi zaidi. Dkt. Tulia ameyasema hayo wakati akichangia kwenye Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa (UNGA79) uliofanyika New York nchini Marekani leo tarehe 22 Septemba, 2024. Katika mchango wake amesisitiza kuwa juhudi za kusaidia nchi zinazoendelea kukuza uchumi zinapaswa kuongozwa na mikakati ya kimkakati, hususan katika kugawanya…
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyoanza leo Septemba 22 na kumalizika kesho Septemba 23, 2022. Akizungumza na Waandishi hao Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki Dkt Zakia aliwataka kuzingatia mafunzo wanayopewa, dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa weledi. Mafunzo hayo ni…
Askofu Ludovick Minde, Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, ateta na walemavu: Katika siku maalum ya Ibada na hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kusali na walemavu kutoka Vikarieti nne za Jimbo, Rombo, Vunjo, Moshi na Hai hapo jana. Askofu Minde katika mahubiri yake alisema zipo aina mbili za ulemavu na Ulemavu unaoonekana na usioonekana. Hivyo walemavu wasijione kuwa wao ni tofauti na watu wengine. Watu wote ni sana. Ameeleza kuwa Ulemavu wao kama wanavyoonekana; sio jambo litakalowanya wajione tofauti na watu wengine. Ni lazima wajiongeze kwa kutokomeza dhana ya utegemezi kwani wakiwezeshwa wanaweza kufanya shughuli za maendeleo katika familia zao.…