Author: Mbeya Yetu

Askofu Robert Pangani wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi amewataka Waumini na Watanzania kwa ujumla kuiombea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuendelea kudumisha amani nchini. Askofu Robert Pangani ametoa wito huo katika ibada maalumu ya mbaraka kwa Mashemasi kumi na sita na Makasisi watatu ibada iliyofanyika Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Ushirika wa Nzovwe kiongozi wa ibada akiwa nia makamu Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Asulumenie Dickson Eva Mwahalende. Amesema hafurahishwi na vitendo vya utekaji na mauaji ya watu yanayoendelea nchini hivyo ameziomba Mamlaka husika kuwabainisha watu hao kuendelea kudumisha amani nchini…

Read More

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea ametoa wito kwa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za rufaa za mikoa Tanzania Bara kwenda kuongeza Ubunifu wa kuanzisha huduma mpya za Kibingwa katika hospitali zao ili wananchi wapate huduma bora za Afya Dkt Nyembea ametoa wito huo leo tarehe 20 Septemba, 2024 jijini Mbeya katika kuhitimisha kikao kazi cha Waganga Wafawidhi, Wauguzi Wafawidhi, Makatibu wa Hospitali na Waratibu wa Ubora wa Huduma(QI) wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Tanzania bara.”Niwaelekeze Kupitia kikao hiki kahakikisheni mnakwenda kuboresha huduma kwa kuanzisha angalau huduma mpya za kubingwa nane katika…

Read More

Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza, ameendelea na ziara yake kwa mara nyingine baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge akikutana na wananchi katika vijiji na kata mbalimbali ili kusikiliza kero zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Mbunge Njeza ameendelea na ziara yake katika vijiji kadhaa vya kata za Iyunga Mapinduzi na Igale.

Akiwa katika kata ya Iyunga Mapinduzi amesikiliza kero za wananchi ambao kwa nyakati tofauti wameshukuru kwa namna miradi inayoendelea kutekelezwa ikiwemo usambazaji huduma ya umeme vijijini, usambazaji huduma ya maji na uboreshaji miundombinu ya elimu licha ya baadhi ya changamoto kuendelea kuwakabili.

Wananchi hao wameeleza kukabiliwa na kadhia ya bei kubwa ya huduma za afya hasa huduma ya upasuaji kwa akina mama.

“Sisi hapa tunamuomba mama yetu ni mwanamke kama sisi tunasikia anamwaga hela kwa Simba na Yanga basi atupunguzie bei za upasuaji na sisi huku maana hata mimi napenda Simba na Yanga”, ameeleza mwananchi wa kata ya Iyunga Mapinduzi Mwile Mboko.

Naye Rashid Fungambili mkazi wa kijiji cha Shuwa katani humo ameomba Serikali kupeleka daktari katika kijiji chao ambacho kina zahanati na kata ina kituo cha afya tarajiwa.

Mbunge Oran Njeza wa Mbeya vijijini, amepokea kero hizo kwa ajili ya kuziwasilisha kwa wataalam kuzitafutia ufumbuzi mara moja ambapo kuhusu huduma za afya kwa ujumla amewashauri wananchi wake kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kupata matibabu hata wasipokuwa na fedha.

Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya ikiwemo kujenga na kuboresha vituo vya afya kuwa vya kimkakati na kwenye kata hiyo amesema kituo cha afya cha kimkakati kitajengwa ili kuhudumia kata za Iyunga Mapinduzi, Isuto na Itawa.

Kero nyingine ni pamoja na barabara hasa kuelekea msimu wa mvua ambapo Mbunge huyo amewaondoa hofu wananchi kwa kumuinua afisa kutoka wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Mbeya ambaye amesema barabara ya Mbalizi Shigamba (Km 52) inaanza kujengwa Oktoba 2024.

Kuhusu barabara ya Iyunga Mapinduzi kwenda Shisonta afisa kutoka wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA Mhandisi Mollel ameipokea na kuahidi TARURA kuiingiza kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha (2025-2026) ili ijengwe kwa kiwango bora.

“Mheshimiwa Mbunge kuhusu barabara hii ya Iyunga Mapinduzi Shisonta naomba nichukue, tutaiingiza kwenye bajeti ya 2025-2026”, ameeleza Mhandisi Mollel.

Pamoja na hayo Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, ameendelea kuhimiza wananchi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao shuleni ambapo katika kila shule aliyopita amechangia shilingi laki mbili ili kuwaunga mkono wananchi hao.

Read More

Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza, ameendelea na ziara yake kwa mara nyingine baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge akikutana na wananchi katika vijiji na kata mbalimbali ili kusikiliza kero zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Mbunge Njeza ameendelea na ziara yake katika vijiji kadhaa vya kata za Iyunga Mapinduzi na Igale. Akiwa katika kata ya Iyunga Mapinduzi amesikiliza kero za wananchi ambao kwa nyakati tofauti wameshukuru kwa namna miradi inayoendelea kutekelezwa ikiwemo usambazaji huduma ya umeme vijijini, usambazaji huduma ya maji na uboreshaji miundombinu ya elimu licha ya baadhi ya changamoto…

Read More

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.  Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida.…

Read More

Sharif Abdul Afisa Mwandamizi kitengo cha mahusiano Jamii na ujirani mwema hifadhi ya Taifa Ruaha amesema kupitia mradi wa REGROW wameandaa Muongozo rafiki wa kupokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi.
Amesema kupitia mradi wa REGROW viongozi na kamati za kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka mkoa wamejengewa uwezo kwa kupewa elimu namna ya kutumia muongozo huo ili kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi. Lengo nikuhakikisha wananchi wanaoathirika na shughuli za hifadhi au Mradi wa REGROW wanawasilisha malalamiko yao na yanashughulikiwa kwa utaratibu unaofahamika.
Aidha Abdul amewasihi wananchi wenye malalamiko wafike ofisi za Serikali ya Kijiji nakuwasilisha malalamiko yao au wapige simu ya bure moja kwa moja kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha namba 0800110801 na Wizara ya Maliasili na Utalii namba 0800110804 endapo lalamiko linahusu Hifadhi au Mradi wa REGROW. Malalamiko yote yatashughulikiwa kwa usiri na mlalamikaji atalindwa na sheria na tararibu za nchi.

Read More

REGROW ni Mradi wa Serikali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa Lengo la kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na hifadhi ya Mikumi, Udzungwa na Nyerere wanatekeleza mradi huu. Kutokana na utekelezaji wa mradi wa REGROW au shughuli za Hifadhi ya Taifa Ruaha, unaweza kuwa na maoni au malalamiko yanayotokana na shughuli hizo. Kila mtu ana nafasi ya kutoa malalamiko yake kuhusu changamoto zinazotokana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na shughuli za Mradi wa REGROW. Iwe malalamiko ya athari zinazotokana na usimamizi wa hifadhi, kero za ardhi, unyanyasaji na…

Read More