Browsing: Video Mpya

Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi Wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson imeandaa Mashindano ya Mapishi kwa Mama na Baba Lishe Mbeya Mjini.

Mashindano hayo ya Mapishi yanajulikana kwa Jina la Tulia Cooking Festival yanatarajiwa Kufanyika Mwishoni mwa Mwezi Agosti Mwaka huu 2024, yakishirikisha Washiriki Elfu Moja (1,000) yenye kauli mbiu isemayo Tumia Nishati Mbadala Kuondoa Uchafuzi wa Mazingira.

Afisa anayeshughulikia malamiko Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Francis Mhina amesema taasisi yake imerahisisha upatikanaji wa ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya mijini na vijijini.

Ameyasema hayo katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya.

Katika hatua nyingine Mhina amesema mwananchi mwenye malalamiko juu ya utendaji usioridhisha kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira,Shirika la Umeme na Vituo vya mafuta ofisi yake ipo wazi kupokea chamoto hizo.
Tobieta Makafu Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo inahudumia Mikoa ya Mbeya,Njombe,Songwe na Rukwa amesema endapo mwananchi atauziwa mafuta kinyume na bei elekezi asisite kutoa taarifa EWURA.

Wananchi Mikoa ya Nyanda za Juu wamejitokeza kwa wingi kutembelea Uwanja wa Maonesho John Mwakamgale hususani katika banda la Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira(NEMC).

Tilika Mwambungu ni Afisa Mazingira Kanda ya Nyanda za Juu Kusini anaeleza elimu wanayoitoa katika banda lao.

Baadhi ya washiriki waliotembelea banda hilo wamefurahishwa na huduma zinazotolewa wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi Scripture Union iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira(NEMC) limetilia mkazo kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na hutumia maonesho mbalimbali kufikisha ujumbe kwa jamii.