Mkuu wa Wilaya ya Songwe amefanya kikao na uongozi wa Kampuni ya Mamba Minerals inayowekeza katika uchimbaji wa madini adimu duniani ya Rare Earth Metals kijiji cha Ngwala Wilayani Songwe.Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, ndugu Godfrey Kawacha kimefanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Mkwajuni.Akizungumza baada ya Kikao hicho, Mhe. Itunda amesema kuwa uongozi huo umemweleza maendeleo ya mchakato wa tathmini na mipango ya kuanza kulipa fidia kwa wananchi.Mkuu huyo wa Wilaya ameusisitiza uongozi huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kila hatua wanayofikia ili wananchi wajue kinachoendelea katika eneo hilo.Pia, DC Itunda amesema kuwa uongozi huo umemweleza kuwa ujenzi wa mgodi huo utaanza Januari, 2025.“Tumefanya kikao na wenzetu wa Mamba, Kampuni ambayo inayowekeza katika uchimbaji wa madini adimu duniani ya Rare Earth Metals kule Ngwala. Kampuni hii wanaanza ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondary Ngwala na Kituo cha Polisi kule Ngwala” amesema DC Itunda.Wawakilishi wa Kampuni hiyo wameongozwa na Mkurugenzi wa Mamba Minerals Corporation Limited ( MML), Ismail Diwani.
Trending
- MAHUNDI AZINDUA VIKOBA DAR ES SALAAM
- MHESHIMIWA MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI AZINDUA KIKUNDI CHA VICOBA DAR ES SALAAM
- Jinsi mume alivyomuokoa mkewe kufanyiwa upasuaji kipindi akijifungua
- SHUHUDIA VIPAJI VYA WANAFUNZI WANAOTARAJIA KUANZA DARASA LA KWANZA 2025 MARYS PRE &PRIMARY SCHOOL
- Hii ndio sababu elimu pekee haiwezi kukusaidia kupata ajira
- CHAUMMA YAGAWA UBWABWA KUSHEREKEA USHINDI WA UENYEKITI WA MTAA
- Nilivyomrejesha mume tuliyeachana kwa talaka
- Viongozi wa Dini Wapongeza Utulivu na Amani Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa