Serikali mkoani Rukwa imekiri kuwepo uzembe katika usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa Vituo vya Afya Viwili na Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga,Mkoani Rukwa, yenye gharama ya shilingi Bilioni 2.6 ambayo imeshindwa kukamilika kama ilivyopanga lakini fedha zote zimekwisha.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA ameendelea na ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya, katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, ambapo imebainika matumizi ya fedha hayalingani na thamani ya fedha iliyotengwa na serikali.
Sendiga amesema mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mollo kilichotengewa shilingi Milioni 400 fedha zimekwisha majengo matano hayajakamilika, Kituo cha Afya cha Matanga kilichopelekewa shilingi Milioni 500 fedha zimeisha majengo hayajakamilika, Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga yua ISOFU iliyotumia shilingi Bilioni 1.8 majengo yake hayajakamilika.
Amesema kuna uzembe ambao umetumika kutekeleza miradi hiyo, na uzembe umejitoikeza katika usimamizi na ufuatiliaji, kwani utekelezaji wa miradi yote hiyo inakwenda kwa mfumo wa Force akaunti, Wananchi hawashirikishi katika utekelezaji wa miradi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga SEBASTIAN WARYUBA naye amekiri watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wamemuangusha kwasababu uzembe huo unawahusu, ikiwemo idara ya uhandisi, idara ya manunuzi na watendaji wengine.
Hata hivyo Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dokta IBRAHIMU ISAACK amebaini ukikwaji wa miongozo ya utekelezaji wa mfumo wa Force akaunti, ambapo ofisi ya manunuzi katika ofisi ya mkurugenzi iliwanunulia vifaa wananchi badala ya wajumbe wa kamati ya ujenzi wa vituo vya afya.
*********************MWISHO*******************
Trending
- Nilikataliwa na Wanaume Wote Lakini Hatua Niliyopiga Ilinifanya Niolewe na Tajiri
- Aibu!! Askofu Mkuu abainika kuiba fedha kanisa lake
- Kongamano la Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050 Kufanyika Mbeya
- Prof. Makulilo: Watanzania Wajiandae kwa Uchumi Jumuishi Kuelekea Dira 2050
- Tajiri wa madini aliyefilisika arejea tena katika biashara kwa kishindo
- Nilirogwa Nipoteze Kila Kitu ila Hatua Niliyopiga Ilinivunja Minyororo Ya Uchawi
- Niliibiwa Gari Yangu Usiku, Lakini Hatua Niliyopiga Ilifanya Wezi Wenyewe Walirudishe Hadi Getini
- Nilipoteza Mume Wangu Kwa Mpango wa Kando ila Kitu Nilichojaribu Kilimfanya Aombe Radhi Hadharani