Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Kila Mwaka Mpya Nilianza na Bahati Mbaya Mwaka Huu Niliingia Nikiwa Tayari

December 30, 2025

Tuligombana Wakati wa Krismasi Mazungumzo Moja Yalizuia Kuvunjika kwa Familia

December 30, 2025

WANANCHI HAI, FUONI , KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO

December 29, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Kila Mwaka Mpya Nilianza na Bahati Mbaya Mwaka Huu Niliingia Nikiwa Tayari
  • Tuligombana Wakati wa Krismasi Mazungumzo Moja Yalizuia Kuvunjika kwa Familia
  • WANANCHI HAI, FUONI , KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO
  • Mume Wangu Alikuwa Akipoteza Udhibiti Usiku na Kukojoa Kitandani Hatua Moja Ilinirejesha Amani Nyumbani
  • Dadangu Aliokota Mchanga Wa Nyayo Zangu Baada Ya Kuenda Kijijini Na Gari Mpya Lakini Maelezo Maalum Yaliniokoa Katika Hofu
  • Mhe. Mahundi: Wazee ni Tunu ya Taifa, Wastahili Kulindwa na Kuheshimiwa
  • NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI
  • Sikuweza Kulala Usiku Juu Ya Ndoto Mbaya Lakini Sasa Nalala Kama Mtoto Baada Ya Kupata Suluhisho
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home ยป RAIS SAMIA HATAKI MISUKOSUKO KWA WAFANYABIASHARA- DKT. BITEKO
Habari za Kitaifa

RAIS SAMIA HATAKI MISUKOSUKO KWA WAFANYABIASHARA- DKT. BITEKO

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMarch 10, 2024Updated:March 10, 20241 Comment8 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.

๐Ÿ“Œ Ataka Watendaji Warasimu wajionee aibu;watimize wajibu

๐Ÿ“Œ Watumishi wakumbushwa shughuli za Serikali kufanyika Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.

Dkt. Biteko amesema hayo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Rafiki Hoteli ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.

Aidha, Dkt. Biteko amewaagiza watendaji wa Serikali kuhakikisha wanailea Sekta binafsi na kila mtu atimize wajibu wake kwenye eneo lake โ€œkama wewe ni Afisa wa TANESCO uliye na wajibu wa kumuunganishia mfanyabiashara umeme ambao mwisho wa siku ataulipia kwa ajili ya mapato yako, huna sababu ya kumwambia njoo kesho wakati kazi hiyo ungeifanya leo.โ€

Amesema Watendaji ambao ni warasimu lazima waone aibu kwa kuchelewesha shughuli zinazoijenga nchi.

Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia anataka kuona watanzania wakiwa kwenye daraja la kwanza katika nchi yao na pia waweze kufanya uwekezaji ndani na nje ya nchi bila vikwazo vyovyote.

Kuhusu Sekta ya Utalii nchini, amesema bado kuna changamoto ya upungufu wa vitanda kwa wageni wa ndani na nje ya nchi hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye sekta ya hospitality ambapo amewapongeza wamiliki wa Rafiki hoteli na wawekezaji wengine ambao wanaifanyia kazi changamoto hiyo.

Vilevile, Dkt. Biteko ameipongeza menejimenti ya hoteli hiyo kwa kutekeleza dhana ya nishati safi ya kupikia kutokana na kuweka miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye hoteli husika na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu mazingira na kutokukata miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesisitiza umuhimu Idara na taasisi mbalimbali Serikalini kutumia miundombinu ya uwekezaji Jijini Dodoma ambayo ndio Makao Makuu ya Nchi.

Kutokana na hilo ameagiza Watendaji wa Serikali kuhakikisha kwamba shughuli zinazoweza kufanyika ndani ya Mkoa wa Dodoma zifanyike katika Mkoa husika ili pia kutoa fursa kwa wanachi kupata huduma muda wote pale wanapohitaji huduma za watendaji hao.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa Rafiki Hoteli Fladmiry Mallya ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji ambayo yanafanya Watanzania kuendelea kuwekeza kwenye nchi yao na hivyo kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kukuza ajira.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

WANANCHI HAI, FUONI , KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO

December 29, 2025

NDELE MWASELELA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI, KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO NA KUWASEMEA WANANCHI

December 29, 2025

MH. MAHUNDI AWAHIMIZA VIJANA KUISHI KWA MISINSI YA UWAJIBIKAJI NA UTU

December 23, 2025

1 Comment

  1. Doncaster escorts on January 22, 2025 6:26 am

    What’s Happening i am new to this, I stumbled upon this I’ve discovered It absolutely helpful and it has helped me out
    loads. I’m hoping to give a contribution & help different customers like its helped me.

    Good job.

    Reply

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025284

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025238

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024212

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025131
Don't Miss
Uncategorized

Kila Mwaka Mpya Nilianza na Bahati Mbaya Mwaka Huu Niliingia Nikiwa Tayari

By Mbeya YetuDecember 30, 20251

Kila mwaka ulipofika mwisho, nilikuwa na wasiwasi badala ya matumaini. Januari kwangu haikuwa mwanzo mpya,…

Tuligombana Wakati wa Krismasi Mazungumzo Moja Yalizuia Kuvunjika kwa Familia

December 30, 2025

WANANCHI HAI, FUONI , KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO

December 29, 2025

Mume Wangu Alikuwa Akipoteza Udhibiti Usiku na Kukojoa Kitandani Hatua Moja Ilinirejesha Amani Nyumbani

December 29, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Kila Mwaka Mpya Nilianza na Bahati Mbaya Mwaka Huu Niliingia Nikiwa Tayari

December 30, 2025

Tuligombana Wakati wa Krismasi Mazungumzo Moja Yalizuia Kuvunjika kwa Familia

December 30, 2025

WANANCHI HAI, FUONI , KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO

December 29, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025284

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025238

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024212
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.