Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Chrysoula Zacharopoulou, Waziri wa Nchi-Maendeleo ya Uchumi (Secretary of State for Economic Development) wa Ufaransa.
Akizungumza malengo na dhamira ya kutoa mualiko kwa Wizara ya Maji Tanzania, Mheshimiwa Chrysoula amesema Serikali ya Ufaransa inatambua na kuthamini jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika dhamira ya kuimarisha huduma ya Maji kwa wananchi na kwamba wanaamini hiki ni kipaumbele chake katika kipindi cha uongozi wake na kusisitiza kwamba katika kuunga mkono jitihada hizo serikali yake ya awamu ya sita Serikali ya Ufaransa imejidhatiti kuwekeza katika miradi ya Maji mingi zaidi kwa kuthamini kazi anayoifanya na pia umuhimu wa sekta kwa maisha ya watu kwani maji ni uhai.
ia, Kiongozi huyo ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa serikali yake kukamilisha Miradi ya Maji Mikubwa na ya Kimkakati na usimamizi mzuri wenye kujali thamani ya fedha na wakati katika pamoja na Miradi ile inayoendelea ambayo inatekelezwa kwa Mashirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo Ufaransa AFD kama Miradi ya Maji miji ya SHINYANGA, MUSOMA, BUKOBA, MWANZA AWAMU YA 1 na MOROGORO AWAMU YA 1 pamoja na Mradi wa Majitaka eneo la Kurasini Jijini DAR ES SALAAM inayofadhiliwa na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo Ufaransa(AFD)
Aidha Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amewasilisha salamu za Shukrani za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji uliofanyika Sekta ya Maji Tanzania na kushukuru kwa Serikali ya Ufaransa kuridhia mapendekezo ambayo Mhe Rais alimuagiza kuwasilisha ikiwa ni pamoja na Utekelezaji wa Mradi wa Maji Chanzo cha Ziwa Victoria Jijini Mwanza Awamu ya pili ya usambazaji maji baada ya ujenzi wa Miundombinu kukamilika, Awamu ya Pili ya Mradi wa Maji Morogoro baada ya awamu ya kwanza inayoendelea ya ujenzi wa Miundombinu kukamilika na ombi liliwasilishwa kwa mara ya kwanza la Utekelezaji wa Mradi wa Maji chanzo cha Ziwa Tanganyika kwa mikoa ya Katavi na Rukwa.
Trending
- Nilinunulia Mtoto Doli Ambayo Ilirudi Kutuhangaisha Sisi Wote, Njia Hii Ndio Iliyotuokoa
- Niliona Watu Wakigeuka Dhidi Yangu Bila Sababu Baadaye Nikagundua Chanzo cha Chuki Isiyoelezeka
- Nilipofahamu Ushirikina Usioonekana Kwenye Familia Yangu, Kila Nilichojuwa Kilikuwa Kinaogopesha
- Kila Nilipopata Pesa, Zilikuwa Zikitoweka Sababu Nilizoigundua Ilinishtua
- Ubishi Wageuka Rekodi: Bodaboda Afika Dar kwa Saa 10
- Huzuni Mbeya: Mwalimu Afia Nyumbani, Mwili Wakutwa Umeharibika Baada ya Wiki Tatu
- Mauaji ya Kikatili Mbeya: Watoto Watatu Wanyongwa kwa Ajili ya Ng’ombe
- Niliona Kila Kitu Kikikwama Nyumbani Mabadiliko Madogo Yalileta Utulivu Uliokosekana

