Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya amewataka wananchi kutotoa taarifa zao za mawasilano kwa watu wasiowafahamu Ili kuepusha matapeli na wezi wa mitandaoni.
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa wito Zanzibar katika ziara yake ya kikazi kukagua minara ya mawasilano na usikivu sanjari na kuboresha miundombinu ya mawasilano.
Aidha amesema Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA)kwa kushirikiana na Wizara wameendelea kutoa elimu na kuchukua hatua dhidi ya matapeli hivyo wananchi wanapopigiwa simu na matapeli watoe taarifa kupitia namba 1504015040 ambapo hatua za haraka zitachukuliwa dhidi yao.
Amesema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Hussein Mwinyi zimeendelea kuboresha mawasiliano kupitia mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) ambapo unaendelea kujenga minara ili kuboresha usikivu hasa maeneo ya pembezoni.