Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Viongozi na Wanachama wa Chama hicho kuyatangaza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maeneo mbalimbali nchini hususani Jimbo la Mbeya mjini ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, barabara n.k
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 23 Disemba, 2024 wakati akizungumza na Wanachama hao katika Mkutano Mkuu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini uliofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Tulia ambapo amesema kuwa ni wajibu wa kila Kiongozi kuhakikisha anawaeleza Waanchi wa eneo lake mambo yanayofanyika na sio kunyamaza kimya.
“Serikali yetu imefanya na inaendelea kufanya kazi kubwa katika maeneo yetu, hivyo basi ni wajibu wetu kama Viongozi kuyasema kwa Wananchi. Yawezekana usiyajue yote ya kitaifa lakini wewe yaseme yaliyo kwenye eneo lako la Utawala watu wayajue na wajue mazuri yanayofanywa kwa ajili yao usikae kimya na kuruhusu watu kusema Serikali haijafanya lolote hapana.” Amesisitiza Dkt. Tulia