Mkuu wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera ametembelea Gereza la Ruanda lililoko Jijini Mbeya na Kuzungumza na wafungwa ikiwa ni Pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
RC Homera amewaasa wafungwa hao kuhakikisha wanajifunza ujuzi mbalimbali wawapo hapo ili watakapopata ridhaa ya kurudi uraiani wautumie kuendesha maisha yao na kuwa walimu wa wengine.
Awali Wakieleza Maombi yao kwa RC Homera wamemuomba awahimize Viongozi wa Serikali kufika gerezani hapo kuwatembelea kwakuwa kufika Kwao wao hupata faraja kuu na kuamini kuwa serikali iko pamoja nao.
“Tunakushukuru sana kwa kuja Mkuu wa Mkoa Mimi nimefika hapa 2015 sijawahi kuona Kiongozi Mkubwa anakuja kututembelea, ujio wako tuna imani kuwa liko tumaini kubwa mbele yetu” amesema mmoja wa Wafungwa.
Mbali na hayo wafungwa pia wamemuomba RC Homera kuwasaidia kumleta Dkt: Tulia Ackson spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Mbeya Mjini kadharika Mganga Mkuu wa Mkoa.
“Mh: tusaidie kumuomba Rais wa mabunge Duniani na Spika Dkt: Tulia Ackson aje atutembelee maana yule ndio Mbunge wetu hata kama hatutokei hapa lakini tayari tuko kwenye Ardhi yake aje atuone”
“Pia Mganga mkuu wa mkoa tunamuomba aje atuone maana tunayo mengi ya kuzungumza naye hasa kuhusu magonjwa mbalimbali yanayotusibu”
Baada ya kusikiliza changamoto hizo Mkuu wa Mkoa ameahidi kuyatendea kazi kwa haraka hasa kuwaleta Viongozi wote sawasawa na maombi yao.
Lakini pia ametoa Kiasi Cha Shilingi Milioni Moja kwaajiri ya Kununua Chakula (nyama) Msaada ambao umeambatana na magodoro yaliyotolewa naM/kit UVCCM Mkoa wa Mbeya Yasin Ngonyani kwa Kushirikiana na mfanyabiashara Achimwene.