Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Namna ya kuimarisha ustawi wa ndoa yako

November 23, 2025

RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA

November 22, 2025

Rungwe Wasaini Mkataba wa Bilioni 2.8 Kujenga Soko la Kisasa la Ndizi

November 22, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Namna ya kuimarisha ustawi wa ndoa yako
  • RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA
  • Rungwe Wasaini Mkataba wa Bilioni 2.8 Kujenga Soko la Kisasa la Ndizi
  • Safari Kuelekea Furaha ya Ndoa Iliyokosekana Kwa Muda Mrefu
  • Badili upepo wa Biashara Yako Hadi Mafanikio
  • Watumishi wazembe hawatakuwa na nafasi-Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba
  • Dkt. Mwigulu: “Mabasi ya Esther Yamechomwa Wakidhani Ni Yangu”
  • Mama Dkt. Samia Atua Arusha atoa neno
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LINDI, MTWARA, RUVUMA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI
Habari za Kitaifa

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LINDI, MTWARA, RUVUMA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJanuary 19, 2025Updated:January 19, 2025No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari akizungumza hii leo Januari 18, 2025 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Lindi ambapo amewataka watendaji hao  kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.  Dkt. Zakia Mohamed Abubakar akizungumza hii leo Januari 18, 2025 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Mtwara ambapo amewahimiza watendaji hao kuhakikisha wanahamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.

 

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira akizungumza hii leo Januari 18, 2025 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya mkoa, mkoani Ruvuma kwa Watendaji wa Halmashauri za Madaba, Namtumbo na Tunduru ambapo amewataka kuwa makini katika kila eneo la usambazaji na utunzaji wa vifaa, mafunzo yote na muda sahihi wa ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikishia wapiga kura.
*******
Na. Mwandishi Wetu
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma wametakiwa kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa
na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
 
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume ambaye
pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omar leo tarehe 18 Januari, 2025 wakati
akifunga mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari ngazi ya mkoa, Mkoani Lindi
ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 
“mnapaswa kutekeleza majukumu mliyopewa kwa
kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume,”
amesema Jaji Asina.
 
Amewaasa watendaji hao kutambua uzito na
umuhimu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari na kwamba elimu na ujuzi walioupata
vitawasaidia kutekeleza kwa nadharia na vitendo yale yote waliyofundishwa.
 
“Mnapaswa kutambua uzito na umuhimu wa zoezi
hili la kitaifa na kwamba baada ya ninyi kufundishwa na kuelekezwa ipasavyo
katika mafunzo haya, elimu na ujuzi mliopata vitawasaidia kutekeleza kwa
nadharia na vitendo yale yote mliyofundishwa,” amesema.
 
Akifunga mafunzo kama hayo mkaoni Mtwara,
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.
Dkt. Zakia Mohamed Abubakar amewahimiza watendaji hao kuhakikisha wanahamasisha
wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba
itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.
 
“Ni matarajio ya Tume kuwa, mara baada ya
zoezi hili kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni wapiga kura
halali.
 
 Jukumu
la uhamasishaji linawahusu moja kwa moja ninyi watendaji, kwa kushirikiana na
wadau wengine katika maeneo yenu kupitia nyenzo mlizo nazo,” amesema Mhe.
Zakia.
 
Mkoani Ruvuma mafunzo hayo yamefungwa na
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira ambaye aliwakumbusha watendaji hao
kuwa makini katika kila eneo la usambazaji na utunzaji wa vifaa, mafunzo yote
na muda sahihi wa ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikishia wapiga kura.
 

Mafunzo hayo yamefanyika
ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari mkoani Mtwara, Lindi na mkoa wa Ruvuma
kwenye Halmashauri za Wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduri  ambapo uboreshaji utafanyika kwa siku saba
kuanzia tarehe 28 Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari, 2025 na vituo
vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

 

Mwenyekiti wa Mafunzo Mkoani Mtwara, Ndg. George Mbogo akizungumza.

 

 
Meza kuu Mkoani Lindi 

 

Watendaji mkoani Mtwara wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo.

 

Mafunzo kwa vitendo mkoani Mtwara

 

 

Watendaji Mkoani Ruvuma wakimsikiliza mgeni rasmi akifunga mafunzo hayo. 

 

Watendaji Mkoani Lindi wakimsikiliza mgeni rasmi akifunga mafunzo hayo. 

 

 

Watendaji Mkoani Lindi wakifanya mafunzo kwa vitendo.

 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA

November 22, 2025

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE

November 21, 2025

VIONGOZI WA BARAZA KUU LA WAISLAMU BAKWATA MKOA WA MBEYA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU JIJINI MBEYA.

November 9, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025228

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025127
Don't Miss
Uncategorized

Namna ya kuimarisha ustawi wa ndoa yako

By Mbeya YetuNovember 23, 20251

Kutana na Joyce ambaye alikuwa mwanamke mwenye bidii kutoka Mkoa wa Manyara, anayejulikana kwa tabasamu…

RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA

November 22, 2025

Rungwe Wasaini Mkataba wa Bilioni 2.8 Kujenga Soko la Kisasa la Ndizi

November 22, 2025

Safari Kuelekea Furaha ya Ndoa Iliyokosekana Kwa Muda Mrefu

November 22, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Namna ya kuimarisha ustawi wa ndoa yako

November 23, 2025

RUNGWE WAINGIA MKATABA WA BILLIONI 1.8 NA KAMPUNI YA KAGWA GENERAL SUPPLIES LIMITED KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA

November 22, 2025

Rungwe Wasaini Mkataba wa Bilioni 2.8 Kujenga Soko la Kisasa la Ndizi

November 22, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025228

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.