Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

VIDEO: ZIARA YA KUSHTUKIZA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA, HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA

November 15, 2025

Kutoka Kupoteza Kazi Hadi Kujiamini Tena Safari Yangu Ya Kurudi Kuwa Mwanaume wa Nyumba

November 15, 2025

Nilivyopata Utajiri Usionisumbua Baada ya Kuacha Kufuata Marafiki Wenye Mashinikizo

November 15, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • VIDEO: ZIARA YA KUSHTUKIZA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA, HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA
  • Kutoka Kupoteza Kazi Hadi Kujiamini Tena Safari Yangu Ya Kurudi Kuwa Mwanaume wa Nyumba
  • Nilivyopata Utajiri Usionisumbua Baada ya Kuacha Kufuata Marafiki Wenye Mashinikizo
  • BAKWATA YATOA TAMKO JUU YA MATUKIO YA OKT 29 SIKU YA UCHAGUZI MKUU LASOMWA KWA WAISLAMU NCHI NZIMA
  • Nilivyofanikiwa Kuacha Kukasirika Haraka na Kuishi Kwa Amani na Watu
  • Nilivyopata Upendo wa Kweli Baada ya Miaka ya Kutumiwa na Kuumizwa
  • Rais Samia Atoa Msamaha kwa Waliojiingiza Kwenye Machafuko Bila Kudhamiria
  • Dkt. Samia Amuapisha Dkt. Mwigulu: Tanzania Yapata Waziri Mkuu Mpya
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » SERIKALI YARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA ZA MTILI–IFWAGI NA WENDA–MGAMA
Habari za Kitaifa

SERIKALI YARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA ZA MTILI–IFWAGI NA WENDA–MGAMA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJanuary 30, 2025No Comments40 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

#Mkandarasi barabara ya Ilula Image-Ilambo atakiwa kurejea kazini mara moja

Iringa

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff, amesema serikali inaridhishwa na kazi zinayofanywa na wakandarasi wanaojenga barabara za Mtili – Ifwagi (Km. 14) na Wenda – Mgama (Km. 19) ambazo zinagharimu bilioni 52.

Barabara hizo zinajengwa chini ya mradi wa RISE, unaofadhiliwa kupitia mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia, ukiwa na lengo la kurahisisha usafirishaji wa mazao ya misitu, mboga mboga, chai, na mazao mengine kutoka mashambani hadi sokoni kwa wakati.

Akizungumza baada ya kuongoza kamati zinazohusika na usimamizi wa mradi huo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi, Mhandisi Seff amesema miradi hiyo ipo katika hatua nzuri na akawataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati uliopangwa ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Aidha, amewataka wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi kuwa walinzi wa kwanza wa barabara hizo ili kuzuia hujuma na wizi unaofanywa na watu wasio waaminifu, jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kwa serikali na kuhatarisha usalama wa miradi hiyo.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Seff ameagiza mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Ilula Image – Ilambo (Km. 40) kurejea kazini mara moja ili kukamilisha kazi hiyo na kuondoa vikwazo vya mawasiliano vilivyopo kwenye barabara hiyo.

Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hii ili kuhakikisha wananchi wananufaika kwa wakati na miundombinu inaboreshwa kwa ufanisi.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VIONGOZI WA BARAZA KUU LA WAISLAMU BAKWATA MKOA WA MBEYA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU JIJINI MBEYA.

November 9, 2025

TUME YATANGAZA WABUNGE 115 WA VITI MAALUM

November 7, 2025

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025229

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025220

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025127
Don't Miss
Video Mpya

VIDEO: ZIARA YA KUSHTUKIZA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA, HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA

By Mbeya YetuNovember 15, 202510

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 15, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuziagiza hospitali zote nchini zihakikishe wajawazito wanapofika hospitali wahudumiwe kwa haraka ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizaya ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali zote nchini ziweke vipaumbele vya kuwa na dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika. “ Haipendezi mwananchi kufika hospitali na kupatiwa vipimo vyote kisha anaambiwa dawa akanunue kwingine, kama duka binafsi linaweza kupata dawa hizo, inawezekanaje hospitali za serikali hapati? Naagiza Hospitali zote ziwe na dawa.”

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi nje ya hospitali hiyo baada ya kutembelea wananchi waliofika hospitalini hapo kupata huduma mbalimbali za kitabibu ambapo amesisitiza wananchi waendelee kuhudumiwa vizuri kwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini vikiwemo vifaa tiba na dawa.

Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu ameziagiza hospitali zote nchini zihakikishe zinakuwa na vifaa vya usafi binafsi vya dharura vikiwemo ndoo na beseni katika wodi za wazazi ili viwasaidie akinamama wasiokuwa na vifaa hivyo. “Ujauzito sio suala la dharura vifaa kama ndoo tunapaswa kuwa navyo katika hospitali zetu za serikali.”

Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika uboreshaji wa huduma za afya nchini. Waziri Mkuu akiwa hospitalini hapo, wananchi walimueleza kuwa wanahudumiwa vizuri na kwa uangalizi wa karibu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wagonjwa na wananchi wanaoguza ndugu zao wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora za afya.

Kutoka Kupoteza Kazi Hadi Kujiamini Tena Safari Yangu Ya Kurudi Kuwa Mwanaume wa Nyumba

November 15, 2025

Nilivyopata Utajiri Usionisumbua Baada ya Kuacha Kufuata Marafiki Wenye Mashinikizo

November 15, 2025

BAKWATA YATOA TAMKO JUU YA MATUKIO YA OKT 29 SIKU YA UCHAGUZI MKUU LASOMWA KWA WAISLAMU NCHI NZIMA

November 14, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

VIDEO: ZIARA YA KUSHTUKIZA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA, HOSPITALI YA RUFAA YA DODOMA

November 15, 2025

Kutoka Kupoteza Kazi Hadi Kujiamini Tena Safari Yangu Ya Kurudi Kuwa Mwanaume wa Nyumba

November 15, 2025

Nilivyopata Utajiri Usionisumbua Baada ya Kuacha Kufuata Marafiki Wenye Mashinikizo

November 15, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025229

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025220

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.