Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji Mkoa wa Tanga yaliyoanza leo Februari 02,2025 na yatakayomalizika Februari 03,2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji Mkoa wa Tanga yaliyoanza leo Februari 02,2025 na yatakayomalizika Februari 03,2025.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira akiwa akita mkutano huo.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Mratibu wa Uandikishaji Mkoa,Maafisa Uandikishaji,Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi,Maafisa Ugavi na Maafisa Tehama wa Halmashauri wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Mratibu wa Uandikishaji Mkoa,Maafisa Uandikishaji,Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi,Maafisa Ugavi na Maafisa Tehama wa Halmashauri wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Na. Mwandishi Wetu
Watendaji wa uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Tanga na Pwani wametakiwa kufanya kazi kwa
weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele ametoa wito huo jijini
Tanga, mkoani Tanga leo Februari 02, 2025 wakati akifungua mafunzo ya watendaji
wa uboreshaji wa daftari ngazi ya mkoa, mkoani humo.
“Baadhi yenu mlibahatika
kushiriki katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za
Tume ikiwemo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika awamu
zilizopita. Kwa kutumia uzoefu mlionao na mafunzo mtakayopatiwa, ninaamini
mtafanya kazi zenu kwa weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi
hili,” Jaji Mwambegele amewaambia watendaji hao.
Amewataka kutumia uzoefu walionao kuwasaidia wenzao
ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi kama hilo ili waweze kutekeleza
majukumu yao kikamilifu.
Akifungua mafunzo kama hayo
Mkoani Pwani, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji
Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk amewaasa watendaji hao kutekeleza majukumu
yao kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji.
“Ni muhimu kutekeleza
majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya
uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa
sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,” amesema
Jaji Mbarouk.
Ameongeza kuwa kutokuwa
makini katika utunzaji wa vifaa hivyo kutapelekea athari kubwa katika
ukamilishaji wa zoezi hilo muhimu, na kwamba wana wajibu wa kuzingatia
maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili waweze kuyafanyia kazi wakati zoezi hilo
la uboreshaji wa daftari litakapokuwa limeanza kwenye maeneo yao.
Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura utafanyika mkoani Tanga na Pwani kwa siku saba kuanzia
tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 02:00
asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Zoezi hilo ambalo
lilizinduliwa mkoani Kigoma mwezi Julai, 2024 limeshakamilika kwenye mikoa 25 ambayo
ni Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu,
Manyara, Dodoma, Singida, Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja,
Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa,
Songwe, Njombe na Ruvuma.