Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 5 Aprili 2025, amefungua kikao cha 39 cha Jukwaa la Wanawake wa Umoja wa Mabunge Duniani kilichofanyika katika Ukumbi wa Opera, Jijini Tashkent, Uzbekistan.
Kikao hicho kinachoadhimisha miaka 40 ya Jukwaa hilo ni kati ya vikao vya kikatiba vya IPU ambavyo hukutanisha Wabunge Wanawake na kukaribisha pia Wanaume kujadili ajenda za usawa wa kijinsia.
Katika Hotuba yake, Dkt. Tulia amelipongeza Jukwaa hilo kwa kazi nzuri ambayo limekuwa likitekeleza kwa kipindi cha miaka 40 katika kuhakikisha Mabunge Wanachana wanafikia Uwiano na usawa wa Kijinsia na kuendelea kuwahusisha Wabunge wanaume katika kufikia malengo ya Jukwaa.