Rais Mstsaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiongozi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore mjini Ouagadougou na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.
Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.