Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amezindua Wakulima Festival 2025, Jojo Mbeya, akisisitiza matumizi ya TEHAMA kuboresha kilimo na kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa maendeleo endelevu ya wakulima.

