Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo

February 8, 2026

TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya

February 8, 2026

New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama

February 8, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo
  • TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya
  • New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama
  • Utengule Usangu Yapata Jezi, Majiko ya Gesi na Msaada wa Kijamii Kutoka kwa Mbunge Ndingo
  • Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya
  • Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H
  • Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee
  • Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » KUUNDWA KWA JAB NI HATUA YA KUIMARISHA NA KUBORESHA SEKTA YA HABARI – MAJALIWA
Habari za Kitaifa

KUUNDWA KWA JAB NI HATUA YA KUIMARISHA NA KUBORESHA SEKTA YA HABARI – MAJALIWA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuApril 29, 2025No Comments12 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu, JAB

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua kadhaa katika kuimarisha na kuboresha sekta ya habari nchini ikiwa ni pamoja na kuunda Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.

Waziri Mkuu amesema hayo leo tarehe 29 Aprili, 2025 wakati akifunga Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Arusha kwa siku mbili.

“Kwenye sekta ya habari na utangazaji, falsafa ya “4Rs” za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alizozibainisha baada ya kuingia madarakani mwezi Machi 2021, imetekelezwa kwa vitendo hususani kwenye eneo la “Reforms” (Mageuzi),” amesema Waziri Mkuu na kuongeza;

“Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza falsafa hii imechukuwa hatua mbalimbali kuimarisha sekta ya habari na utangazaji nchini kwa kuunda chombo kipya cha kushughulikia usajili wa taaluma ya waandishi wa habari yaani Bodi ya Ithibati”.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari iliyozinduliwa mwaka huu ina jukumu la kusimamia viwango vya kitaaluma kwa wanahabari ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria chini ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.

Amesema hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni kuhakikisha inawezesha shirika la Habari la utangazaji kuwepo kisheria pamoja na kuimarisha Idara ya Habari Maelezo kwa kununua vitendea kazi vikiwemo Magari na vifaa vya kurushia matangazo mbashara.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu inayosema “Uhabarishaji kwenye Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba katika uhuru wa vyombo vya habari” inalenga kujadili athari za teknolojia ya akili mnemba katika uendeshaji wa vyombo vya Habari na uhuru wake.

Amesema Serikali katika kuhakikisha Akili Mnemba (AI) inatumika kwa njia inayowezesha badala ya kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari, imeanzisha mchakato wa kuandaa sera maalum ya AI na waandishi wanaowajibu wa kuchangia ili kupata sera nzuri.

“Sera hii itatoa mwongozo wa matumizi ya AI katika vyombo vya habari, ili kuhakikisha kwamba teknolojia mpya zinaendana na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari, uwazi, na uadilifu wa uandishi wa Habari, hivyo mtumie muda wenu hapa kujadili na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera hiyo,” amesema Waziri Mkuu.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya

January 31, 2026

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAFUNGUA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 KWA MATEMBEZI YA AMANI – MBEYA MJINI

January 30, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025333

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025139
Don't Miss
Video Mpya

Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo

By Mbeya YetuFebruary 8, 20263

TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya

February 8, 2026

New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama

February 8, 2026

Utengule Usangu Yapata Jezi, Majiko ya Gesi na Msaada wa Kijamii Kutoka kwa Mbunge Ndingo

February 7, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo

February 8, 2026

TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya

February 8, 2026

New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama

February 8, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025333

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.