Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilijaribu Kila Njia Kuokoa Uhusiano Wangu Ulioathirika na Pombe Hii Njia Ilifanya Kila Kitu Rahisi

December 24, 2025

Ulinzi Mkali Waimarishwa Kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya 2026 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya

December 24, 2025

MSHTUKO MBEYA: MTOTO DARASA LA SABA AUAWA KWA KIPANDE CHA MTI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAYAI

December 23, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilijaribu Kila Njia Kuokoa Uhusiano Wangu Ulioathirika na Pombe Hii Njia Ilifanya Kila Kitu Rahisi
  • Ulinzi Mkali Waimarishwa Kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya 2026 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
  • MSHTUKO MBEYA: MTOTO DARASA LA SABA AUAWA KWA KIPANDE CHA MTI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAYAI
  • Nilipoteza Amani Bila Sababu Inayoonekana Ufafanuzi wa Kienyeji Ulinipa Mwanga
  • MH. MAHUNDI AWAHIMIZA VIJANA KUISHI KWA MISINSI YA UWAJIBIKAJI NA UTU
  • Familia Yetu Ilikosa Baraka ya Utulivu Tulipoelewa Chanzo, Njia Ikafunguka
  • Tulikaa Ndoa Bila Amani Mazungumzo Moja Yalibadili Mwelekeo Wetu
  • Maumivu ya Ghafla Yalinifanya Nidhani Ni Mwisho, Baadaye Nikagundua Mawe ya Figo Yanatibika Kwa Mitishamba
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » SERIKALI ITAFANYIA KAZI HARAKA MAAZIMIO YA KONGAMANO LA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI- MSIGWA.
Uncategorized

SERIKALI ITAFANYIA KAZI HARAKA MAAZIMIO YA KONGAMANO LA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI- MSIGWA.

Mbeya YetuBy Mbeya YetuApril 29, 2025Updated:April 29, 2025No Comments8 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Wadau na Waandishi wa Habari wakifuatilia uwasilishaji wa mada na majadiliano katika siku ya kwanza ya Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lililofanyika leo tarehe 28 Aprili, 2025 jijini Arusha.

 

 

Na Mwandishi Wetu.
 
Serikali imesema itahakikisha inafanyia kazi mapendekezo yote yatakayotolewa kwenye maazimio ya pamoja ya Waandishi wa Habari baada ya kuhitimisha Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka 2025.
 
Hakikisho hilo la Serikali limetolewa leo tarehe 28 Aprili, 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson wakati akitoa neno la kufunga Siku ya Kwanza ya Kongamano hilo linalofanyika jijini Arusha kwa uratibu wa Jamii Africa, UNESCO na Wizara yenyewe.
 
“Nimesikia maazimio ya awali mliyoyatoa hapa, ni muhimu sana na mimi nitaomba mkishakamilisha ile nakala ya mwisho mtupatie ili na sisi serikalini yale ambayo tunatakiwa tuchukue hatua tuyafanyie kazi, basi tutafanyia kazi mara moja”, amesema Msigwa.
Amewapongeza wadau wote walioshiriki Kongamano hilo na kwa majadiliano waliyoyafanya ikiwemo suala la matumizi ya Akili Mnemba kwa kuwa ni jambo muhimu kwenye kazi za uandishi wa habari kwa sasa. 
 
Bw. Msigwa amesema Serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari nchini na kwamba hilo linajidhihirisha kwani kumekuwa na mazingira rafiki kwa Waandishi wa Habari pale wanapotekeleza majukumu yao.
 
“Sisi Waandishi wa Habari kwenye Awamu hii ya sita tumekuwa tukifanya kazi katika mazingira rafiki sana, kwa sababu ya maelekezo ambayo Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) anayasimamia,” amesisitiza Msigwa na kuongeza;
 

“Aliyoyasema tangu siku ya kwanza alipoingia madarakani ndiyo anayoyatekeleza na sisi lazima tutekeleze maelekezo yake kuhakikisha kuna uhuru wa vyombo vya habari, kuhakikisha waandishi wa Habari hawabughudhiwi lakini kuendelea kujenga mazingira bora kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao.”

Kongamano hilo la Maadhimisho ya Siku ya Siku ya Uhuru wa Habari linatarajiwa kufungwa kesho tarehe 29 Aprili, 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Nilijaribu Kila Njia Kuokoa Uhusiano Wangu Ulioathirika na Pombe Hii Njia Ilifanya Kila Kitu Rahisi

December 24, 2025

Nilipoteza Amani Bila Sababu Inayoonekana Ufafanuzi wa Kienyeji Ulinipa Mwanga

December 23, 2025

Familia Yetu Ilikosa Baraka ya Utulivu Tulipoelewa Chanzo, Njia Ikafunguka

December 23, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025271

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025237

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024211

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025131
Don't Miss
Uncategorized

Nilijaribu Kila Njia Kuokoa Uhusiano Wangu Ulioathirika na Pombe Hii Njia Ilifanya Kila Kitu Rahisi

By Mbeya YetuDecember 24, 20250

Nilihisi uhusiano wangu ulikuwa umekwama kabisa. Mume wangu alikua mnywaji, na kila jaribio langu la…

Ulinzi Mkali Waimarishwa Kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya 2026 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya

December 24, 2025

MSHTUKO MBEYA: MTOTO DARASA LA SABA AUAWA KWA KIPANDE CHA MTI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAYAI

December 23, 2025

Nilipoteza Amani Bila Sababu Inayoonekana Ufafanuzi wa Kienyeji Ulinipa Mwanga

December 23, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilijaribu Kila Njia Kuokoa Uhusiano Wangu Ulioathirika na Pombe Hii Njia Ilifanya Kila Kitu Rahisi

December 24, 2025

Ulinzi Mkali Waimarishwa Kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya 2026 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya

December 24, 2025

MSHTUKO MBEYA: MTOTO DARASA LA SABA AUAWA KWA KIPANDE CHA MTI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAYAI

December 23, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025271

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025237

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024211
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.