Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Mwaselela, amekabidhi vyerehani viwili kwa vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mbeya Mjini ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kuhamasisha uzalishaji wa ndani.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, MNEC Mwaselela alieleza kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya chama ya kujenga vijana waadilifu, wachapakazi na wenye kujitegemea. Alisisitiza kuwa uwezeshaji wa vitendea kazi ni kichocheo muhimu katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Viongozi wa UVCCM pamoja na wanachama walitoa shukrani kwa mchango huo na kuahidi kuvitumia vyerehani hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.