Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji

February 13, 2026

RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

February 11, 2026

CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.

February 11, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji
  • RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya
  • CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.
  • DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji
  • KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA
  • Wilaya ya Mbeya Yapiga Marufuku Kilimo na Ukataji Miti Kwenye Vyanzo vya Maji
  • Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo
  • TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025
Habari za Kitaifa

TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMay 12, 2025No Comments22 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Lusaka, Zambia – Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule, amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, waliofika Ubalozini leo tarehe 12 Mei, 2025 asubuhi kwa ajili ya kujitambulisha. Wataalamu hao wapo nchini Zambia kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa Hospitali ya Kufundishia ya Zambia (University Teaching Hospital – UTH) kuhusu huduma ya uchujaji wa damu kwa njia tumbo (Peritoneal Dialysis).

Katika mazungumzo yake na ujumbe huo Mhe. Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule aliwakaribisha wataalamu hao waliobeba bendera ya Tanzania, akisema kuwa ni fursa muhimu kwa nchi yetu kushiriki katika kubadilishana utaalamu wenye lengo la kuboresha huduma za afya Barani Afrika. Pia, ameshukuru na kupongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasan kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya nchini Tanzania.

“Nawashukuru mmekuja hapa Zambia na mmeona wenyewe na mtafanya ulinganifu, tunayo haki ya kupongeza Serikali ya Tanzania kwa maboresho makubwa katika sekta ya afya yenye nia ya kutoa huduma bora na za kibobezi kwa wananchi wetu pamoja na mataifa jirani. Hii imeifanya Tanzania kuwa kimbilio la nchi nyingi za ukanda wa SADC zinazohitaji huduma za kibingwa na bobezi, hususan katika masuala ya uchujaji wa damu na huduma za magonjwa sugu,” alisema Mhe. Balozi Lt Gen Mkingule.

Ameongeza kuwa, “Huduma hizi zimeboreshwa sana, ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo maalum vya huduma za afya kuanzia ngazi ya Vituo vya Afya, Zahanati, Hospitali kwa kuimarisha miundombuni ya kutolea huduma za afya, ununuzi na ufungaji wa vifaa tiba vya kisasa, pamoja na kuwajengea wataalamu uwezo wa ndani na wa kimataifa. Hii inatoa mwanga wa matumaini kwa wananchi wa Tanzania na jirani zao.” – Mhe. Balozi Lt Gen Mkingule.

Kwa upande wake, Kiongozi wa timu hiyo ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , Dkt. Octaben Kasanga, Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya figo, amemshukuru Mhe. Balozi Lt Gen Mkingule kwa ushirikiano na mapokezi mazuri waliyopatiwa kutoka kwake na Maafisa wa Ubalozi. Timu hiyo ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za tiba na sekta ya afya kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

“Tunashukuru sana Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Wizara ya Afya, Ubalozi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwezesha kushiriki mafunzo haya muhimu katika Hospitali ya Taifa ya Zambia. Lengo letu ni kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na mbinu bora za uchujaji wa damu kwa njia tumbo, ili tuweze kuboresha huduma zetu nyumbani Tanzania,” amesema Dkt. Kasanga.

Amesema kuwa hii ni hatua nyingine muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya afya, ambapo Tanzania inaendelea kuonesha njia ya kuwaweka wananchi wake na nchi jirani katika mstari wa mbele wa huduma bora za kibingwa.

Ziara hii ya mafunzo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia WIzara ya Afya na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kuhakikisha inawaendeleza Watumishi wa Seta ya Afya ndani na nje ya nchi ili waweze kutoa huduma za afya zenye viwango vya kimataifa, na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya katika ukanda wa SADC.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA

February 10, 2026

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya

January 31, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025342

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024229

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025139
Don't Miss
Video Mpya

Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji

By Mbeya YetuFebruary 13, 20263

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Region, Beno Malisa, amesema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza mkoani humo ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa tawi la Strategies Insurance, kampuni inayotoa huduma za bima, uliofanyika jijini Mbeya. Amepongeza uamuzi wa kampuni hiyo kufungua tawi katika mkoa huo, akieleza kuwa hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi na wafanyabiashara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Strategies Tanzania, Jabiri Kigoda, amesema kampuni hiyo imejipanga kutoa huduma bora, za haraka na zinazoendana na mahitaji ya wateja.

Aidha, baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wamewahimiza wananchi kujiunga na huduma za bima ili kujikinga na athari za majanga yanayoweza kujitokeza, pamoja na kulinda mali na maisha yao.

RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

February 11, 2026

CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.

February 11, 2026

DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji

February 10, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji

February 13, 2026

RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

February 11, 2026

CRDB YAUNGANA NA JESHI LA POLISI MBEYA KUELEKEA SIKU MAALUM YA POLISI.

February 11, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025342

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024229
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.