Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Miguu na Mgongo Kwa Muda Mrefu Bila Tiba Kufanya Kazi

November 12, 2025

Nilivyorejesha Hisia Zangu Baada ya Muda Mrefu Bila Kutamani Tena Kuwa Karibu na Mume Wangu

November 12, 2025

BABALEVO AINGIA KWENYE 18 ZA SPIKA ZUNGU AKILA KIAPO BUNGENI

November 11, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Miguu na Mgongo Kwa Muda Mrefu Bila Tiba Kufanya Kazi
  • Nilivyorejesha Hisia Zangu Baada ya Muda Mrefu Bila Kutamani Tena Kuwa Karibu na Mume Wangu
  • BABALEVO AINGIA KWENYE 18 ZA SPIKA ZUNGU AKILA KIAPO BUNGENI
  • Nilivyofanikiwa Kuwatoa Watoto Wangu Kwenye Uraibu wa Simu na Kuwarudisha Kwenye Masomo
  • Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Tumbo Kila Siku Bila Kujua Chanzo
  • Nilivyolipa Madeni Yote na Kuanzisha Biashara Mpya Bila Kukopa Popote
  • Nilivyofanikiwa Kumaliza Migogoro Kati ya Watoto Wangu na Kurudisha Upendo Nyumbani
  • Nilivyopata Kazi Ndoto Zangu Baada ya Kuacha Kusema “Sina Bahati” Kila Wakati
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATENDAJI UCHAGUZI WATAKIWA KUFANYA VIKAO NA VYAMA VYA SIASA
Habari za Kitaifa

WATENDAJI UCHAGUZI WATAKIWA KUFANYA VIKAO NA VYAMA VYA SIASA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 23, 2025No Comments17 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.  (Picha na INEC).

 

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.  (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Mafunzo Ndg. Faustine Lagwen, akizungumza jambo.

 

Washiriki wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo. 

 

Washiriki kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.

Na. Mwandishi wetu.
Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi imewaelekeza watendaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kufanya vikao na
viongozi wa vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa uteuzi wa wagombea unafanyika kwa mujibu wa sheria.


Maelekezo hayo yametolewa na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs
Mwambegele wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi mkoani Shinyanga
leo Julai 23, 2025.

“Mtatakiwa kuyatafsiri mafunzo haya kwenye usimamizi wenu
wa shughuli za kila siku za masuala ya uchaguzi kwa kuanza na vikao na vyama
vya siasa, utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge
na kuhakikisha utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wenyewe ngazi ya udiwani
ufanyike kwa mujibu wa sheria,”
amesema.

Amewaelekeza kuitisha na kuratibu kamati za upangaji wa ratiba za kampeni
na kuitisha kamati za maadili iwapo kuna changamoto zitajitokeza wakati wa kampeni.

Jaji Mwambegele
amewakumbusha watedaji hao kuhusu wajibu wao wa kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa
uchaguzi ngazi ya vituo na kuratibu na kusimamia vizuri na kwa weledi uchaguzi
ngazi ya vituo.

“Mafunzo mtakayowapa yatawawezesha kuratibu na kusimamia
uchaguzi ngazi ya kata vizuri na kwa weledi. Hivyo, jukumu lenu ni kutoa
mafunzo sahihi, kwa kuonesha kwa vitendo yote wanavyotakiwa kuyafanya
wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata,” amesema.

Akifunga mafunzo kama hayo Kisiwani Pemba, Zanzibar, Makamu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mstaafu)
Mbarouk Salim Mbarouk amewakumbusha watendaji hao wajibu wao wa k
ubandika mabango, orodha ya majina ya wapiga kura na
matangazo au taarifa zinazopaswa kuwafikia wapiga kura kwa kuwa ni takwa la
kisheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi.

“Ni wajibu wenu kuhakikisha mabango, matangazo, orodha ya majina ya wapiga
kura na taarifa yoyote inayotakiwa kubandikwa kulingana na kalenda ya
utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi inabandikwa ili kuepusha malalamiko ya ukiukwaji
wa masharti ya sheria na kanuni za uchaguzi,” amesema.

Amewasisitiza watendaji hao kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya
habari ili kuwajulisha wananchi na wadau mambo mbalimbali ya uchaguzi.

“Hakikisheni mnajiandaa kabla ya kukutana na vyombo vya habari. Pima
taarifa yako unayotaka kuitoa kabla hujaitoa ili kuepuka kuleta taharuki badala
ya utulivu katika eneo lako na Taifa kwa ujumla,” amesema.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa
siku tatu kwenye mikoa mbalimbali nchini na yanawajumuisha waratibu wa
uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya
jimbo.

Tume iliyagawa mafunzo hayo
kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya pili ilihusisha mikoa ya Simiyu,
Shinyanga, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Mwanza, Mara, Dar es Salaam, Pwani,
Rukwa, Katavi, Manyara, Arusha, Songwe na Mbeya.

Awamu ya kwanza ilifanyika
tarehe 15 hadi 17 na ilihusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida,
Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera,
Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.
Mwisho.
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VIONGOZI WA BARAZA KUU LA WAISLAMU BAKWATA MKOA WA MBEYA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU JIJINI MBEYA.

November 9, 2025

TUME YATANGAZA WABUNGE 115 WA VITI MAALUM

November 7, 2025

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025226

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025215

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024197

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025126
Don't Miss
Uncategorized

Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Miguu na Mgongo Kwa Muda Mrefu Bila Tiba Kufanya Kazi

By Mbeya YetuNovember 12, 20252

Kwa miaka mingi nilikumbana na maumivu makali miguu na mgongo. Kila hatua nilipokuwa nikitembea, nilihisi…

Nilivyorejesha Hisia Zangu Baada ya Muda Mrefu Bila Kutamani Tena Kuwa Karibu na Mume Wangu

November 12, 2025

BABALEVO AINGIA KWENYE 18 ZA SPIKA ZUNGU AKILA KIAPO BUNGENI

November 11, 2025

Nilivyofanikiwa Kuwatoa Watoto Wangu Kwenye Uraibu wa Simu na Kuwarudisha Kwenye Masomo

November 11, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Miguu na Mgongo Kwa Muda Mrefu Bila Tiba Kufanya Kazi

November 12, 2025

Nilivyorejesha Hisia Zangu Baada ya Muda Mrefu Bila Kutamani Tena Kuwa Karibu na Mume Wangu

November 12, 2025

BABALEVO AINGIA KWENYE 18 ZA SPIKA ZUNGU AKILA KIAPO BUNGENI

November 11, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025226

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025215

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024197
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.