Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilipofahamu Ushirikina Usioonekana Kwenye Familia Yangu, Kila Nilichojuwa Kilikuwa Kinaogopesha

January 17, 2026

Kila Nilipopata Pesa, Zilikuwa Zikitoweka Sababu Nilizoigundua Ilinishtua

January 17, 2026

Ubishi Wageuka Rekodi: Bodaboda Afika Dar kwa Saa 10

January 17, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilipofahamu Ushirikina Usioonekana Kwenye Familia Yangu, Kila Nilichojuwa Kilikuwa Kinaogopesha
  • Kila Nilipopata Pesa, Zilikuwa Zikitoweka Sababu Nilizoigundua Ilinishtua
  • Ubishi Wageuka Rekodi: Bodaboda Afika Dar kwa Saa 10
  • Huzuni Mbeya: Mwalimu Afia Nyumbani, Mwili Wakutwa Umeharibika Baada ya Wiki Tatu
  • Mauaji ya Kikatili Mbeya: Watoto Watatu Wanyongwa kwa Ajili ya Ng’ombe
  • Niliona Kila Kitu Kikikwama Nyumbani Mabadiliko Madogo Yalileta Utulivu Uliokosekana
  • Bosi Wangu Alitaka Kuniangamiza Kwenye Kazi, Lakini Hatua Niliyopiga Ilimfanya Aniombe Msamaha
  • Sikia Mchungaji huyu alivyosema na Wachawi(ABHALOSI KUFWINA INYAMA ZA BHAANDU MUUNDA MMYABHO)
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » UJUMBE WA HELEN KELLER WAFIKA KITUO CHA AFYA ISMANI KUJIONEA ZOEZI LA HUDUMA YA UPASUAJI MTOTO WA JICHO
Habari za Kitaifa

UJUMBE WA HELEN KELLER WAFIKA KITUO CHA AFYA ISMANI KUJIONEA ZOEZI LA HUDUMA YA UPASUAJI MTOTO WA JICHO

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 6, 2025Updated:August 6, 2025No Comments38 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Ujumbe wa Bodi ya Shirika la Kimataifa la Helen Keller tarehe 5 Agosti, 2025 pamoja na masuala mengine ulifika Isman Wilaya ya Iringa kujionea kwa vitendo zoezi linaoendelea la kambi ya upasuaji wa ugonjwa wa macho ujulikanao kama mtoto wa jicho kambi itakayo toa huduma hiyo kwa siku saba.

Akiongea wakati wa kikao kifupi ofisi ya mkuu wa mkoa mkoani Iringa kabla ya kutembelea kituo hicho, Rais wa shirika hilo Sarah Bochie amesema shirika hilo limeamua kutembelea mkoani Iringa ili kujionea na kujiridhisha huduma zinazotolewa kwa vitendo kwani shirika lake linafanya kazi kwa kanzi data na takwimu ili kutoa tathimini ya huduma zake.

Kambi hiyo ya upasuaji mtoto wa jicho inaendelea kwa siku ya nne sasa na inafanya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa takribani wagonjwa 120 kwa siku katika zoezi linaloendeshwa na Madaktari Bingwa kutoka hospitali za nyanda za juu kusini ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James wakati akikaribisha ujumbe wa Bodi ya Wataalam kutoka Helen Keller Ofisini kwake ameshukru shirika la Helen Keller kwa kutoa msaada wa vifaa kila vinapohitajika, kutoa utaalam kwa madaktari wenyeji na kuendeleza ushirikiano kati yao na serikali.

Aidha Mhe. Kheri James amesema lengo la ujumbe wa Helen Keller Mkoani Iringa ni kujionea namna gani huduma wanazofadhili zinavyofanya kazi ikiwemo kujadiliana kwa pamoja maeneo mengine ya ushirikiano kwani shirika hilo limekuwepo hapa nchini kwa zaidi ya miaka 30.

Kufuatia uwepo wa zoezi hilo katika Kituo cha Afya Ismani idadi kubwa ya wanachi wenye shida ya tatizo la mtoto wa jicho imeendelea kujitokeza ili kupata tiba hiyo huku wagonjwa wengi wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wakiwa wanaongoza kwa kuwa na uoni hafifu hivyo kufanya idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa kufanyiwa upasuaji kwa wingi.

Dkt. Stephen Nyamsae Daktari Bingwa wa macho amesema ugonjwa wa mtoto wa jicho ni ukungu unaotokea katika kioo cha ndani ya jicho kutokana na kuongezeka kwa umri hasa kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 50 ambao taratibu hupoteza uwezo wa kuona.

Dkt. Nyamsae anayataja makundi mengine kuwa ni watoto wanaozaliwa na mtoto wa jicho kwasababu kabla ya kuzaliwa kioo hiki hushindwa kujitengeneza, kundi lingine analitaja kuwa ni la watu wenye ugonjwa wa kisukari lakini pia watu wanaopata majeraha katika jicho kutokana na ajali.
Zoezi la Kambi ya Upasuaji wa mtoto wa jicho linaendelea kwa siku 7 likitarajia kuhitimishwa tarehe 9 Agosti mwaka huu hivyo Wananchi waendelee kujitokeza kutumia fulsa hii kwani huduma hii inatolewa bure na imedhaminiwa na shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la Helen Keller.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Child Support Tanzania Yawawezesha Madiwani Mbeya Kuhusu Elimu Jumuishi

January 8, 2026

NMB Yaimarisha Ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya

January 7, 2026

MHE. MAHUNDI AWASISITIZA WATOTO WA SHULE YA MAADILISHO IRAMBO KUBADILIKA NA KUJENGA MUSTAKABALI MWEMA

January 6, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025304

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025243

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024217

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025135
Don't Miss
Uncategorized

Nilipofahamu Ushirikina Usioonekana Kwenye Familia Yangu, Kila Nilichojuwa Kilikuwa Kinaogopesha

By Mbeya YetuJanuary 17, 20263

Kwa muda mrefu nilikuwa nikiishi maisha ya kawaida juu juu. Kila kitu kilionekana sawa. Lakini…

Kila Nilipopata Pesa, Zilikuwa Zikitoweka Sababu Nilizoigundua Ilinishtua

January 17, 2026

Ubishi Wageuka Rekodi: Bodaboda Afika Dar kwa Saa 10

January 17, 2026

Huzuni Mbeya: Mwalimu Afia Nyumbani, Mwili Wakutwa Umeharibika Baada ya Wiki Tatu

January 16, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilipofahamu Ushirikina Usioonekana Kwenye Familia Yangu, Kila Nilichojuwa Kilikuwa Kinaogopesha

January 17, 2026

Kila Nilipopata Pesa, Zilikuwa Zikitoweka Sababu Nilizoigundua Ilinishtua

January 17, 2026

Ubishi Wageuka Rekodi: Bodaboda Afika Dar kwa Saa 10

January 17, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025304

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025243

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024217
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.