Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa Agosti 22, 2025 amemkabidhi boti moja mpya PB.44 ULINZI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga. Akikabidhi boti hiyo kwa Jeshi Mkoa wa Mbeya, Mhe Malisa amelitaka Jeshi hilo kulitumia vizuri boti hilo katika kuimarisha doria za ziwa nyasa Wilayani Kyela na kutokomeza uhalifu. nipe vichwa vitano vya habari Aidha, Mhe.Malisa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa kutimiza ahadi ya kutoa boti kwa ajili ya kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa na kuahidi kuitunza na kuitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa. Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema kuwa Boti hiyo inakwenda kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa kupitia doria za pamoja za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, JWTZ, Uhamiaji na TRA. Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa makuu nchini ambalo sehemu ya Ziwa hilo ni nchi jirani ya Malawi na Mkoa wa Njombe na Ruvuma hivyo uwepo wa Boti hiyo ni mikakati ya kuimarisha ulinzi na kudhibiti uhalifu wa majini.
Trending
- Nilipofahamu Ushirikina Usioonekana Kwenye Familia Yangu, Kila Nilichojuwa Kilikuwa Kinaogopesha
- Kila Nilipopata Pesa, Zilikuwa Zikitoweka Sababu Nilizoigundua Ilinishtua
- Ubishi Wageuka Rekodi: Bodaboda Afika Dar kwa Saa 10
- Huzuni Mbeya: Mwalimu Afia Nyumbani, Mwili Wakutwa Umeharibika Baada ya Wiki Tatu
- Mauaji ya Kikatili Mbeya: Watoto Watatu Wanyongwa kwa Ajili ya Ng’ombe
- Niliona Kila Kitu Kikikwama Nyumbani Mabadiliko Madogo Yalileta Utulivu Uliokosekana
- Bosi Wangu Alitaka Kuniangamiza Kwenye Kazi, Lakini Hatua Niliyopiga Ilimfanya Aniombe Msamaha
- Sikia Mchungaji huyu alivyosema na Wachawi(ABHALOSI KUFWINA INYAMA ZA BHAANDU MUUNDA MMYABHO)

