Mbunge Mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Mh. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amezindua kampeni za CCM Kata ya Mbugani, Wilaya ya Chunya, ambapo aliwaomba wananchi kumpa kura za heshima Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge Jimbo la Lupa Masache Kasaka na Mgombea Udiwani Bosco Mwanginde. Mahundi alisema Dkt. Samia ni kiongozi shupavu aliyeendeleza miradi ya awamu ya tano na kuanzisha mipya kwa manufaa ya wananchi. Naye Bosco Mwanginde aliwashukuru wanachama kwa kumchagua na kuwataka kushirikiana naye katika kuwaletea maendeleo.
Trending
- Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya
- TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA
- AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
- SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN
- EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50
- Kanisa la Moravian Tanzania Lamkabidhi Yona Sonelo Tuzo Maalum Baada ya Shahada ya Heshima Australia
- Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji
- RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

