Mkazi wa Mtaa wa Block “T” uliopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya, Austack Mushi, ameomba Serikali ya Mkoa wa Mbeya kuingilia kati na kumsaidia kurejesha mali na fedha zake zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100, baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana mnamo Septemba 30, mwaka huu.

