Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Tumbo Kila Siku Bila Kujua Chanzo

November 10, 2025

Nilivyolipa Madeni Yote na Kuanzisha Biashara Mpya Bila Kukopa Popote

November 10, 2025

Nilivyofanikiwa Kumaliza Migogoro Kati ya Watoto Wangu na Kurudisha Upendo Nyumbani

November 9, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Tumbo Kila Siku Bila Kujua Chanzo
  • Nilivyolipa Madeni Yote na Kuanzisha Biashara Mpya Bila Kukopa Popote
  • Nilivyofanikiwa Kumaliza Migogoro Kati ya Watoto Wangu na Kurudisha Upendo Nyumbani
  • Nilivyopata Kazi Ndoto Zangu Baada ya Kuacha Kusema “Sina Bahati” Kila Wakati
  • VIONGOZI WA BARAZA KUU LA WAISLAMU BAKWATA MKOA WA MBEYA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU JIJINI MBEYA.
  • Nilivyoshinda Bet Kubwa ya Ligi Kuu Uingereza
  • Nilivyolazimika Kuacha Kazi Nzuri Ili Kuhifadhi Ndoa Yangu Isivunjike
  • TUME YATANGAZA WABUNGE 115 WA VITI MAALUM
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » Shirika la Posta Laadhimisha Wiki ya Posta Duniani kwa Kutoa Msaada Hospitali ya Igawilo
Habari za Kitaifa

Shirika la Posta Laadhimisha Wiki ya Posta Duniani kwa Kutoa Msaada Hospitali ya Igawilo

Mbeya YetuBy Mbeya YetuOctober 9, 2025Updated:October 9, 2025No Comments39 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Shirika la Posta Tanzania (TPC) kupitia Ofisi yake ya Mkoa wa Mbeya, limeadhimisha Wiki ya Posta Duniani kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kukabidhi msaada wa vyandarua katika Hospitali ya Wilaya ya Igawilo, Jijini Mbeya.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Mbeya, Amos Millinga, alisema kuwa wiki hiyo imelenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za Posta, sambamba na kuadhimisha Siku ya Posta Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Oktoba.

“Wiki hii tumeendesha programu maalum inayolenga kutoa uelewa wa huduma zetu za Posta. Lakini sambamba na hilo, tunasherehekea Siku ya Posta Duniani kwa kujihusisha na shughuli za kijamii kama njia ya kurudisha fadhila kwa jamii,” alisema Millinga.

Millinga aliongeza kuwa Shirika la Posta ni miongoni mwa mashirika ya umma yanayojali ustawi wa jamii, na kila mwaka limekuwa likitenga sehemu ya bajeti yake kusaidia sekta za afya, elimu na mazingira.

“Tumeamua kufika hapa Hospitali ya Igawilo kukabidhi vyandarua ambavyo vitasaidia wagonjwa na wadau mbalimbali wanaopokea huduma katika hospitali hii. Tunafanya hivi kama sehemu ya kujali na kuchangia maendeleo ya jamii,” aliongeza Meneja huyo.

Kwa upande wake, Afisa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igawilo, Donald Mwashtete, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo pamoja na Mganga Mkuu wa Jiji la Mbeya, aliishukuru Shirika la Posta kwa kitendo hicho cha kuikumbuka hospitali yao.

“Tunawashukuru sana wenzetu wa Shirika la Posta kwa kutukumbuka na kufanya jambo hili jema. Ni ishara ya upendo na ushirikiano mzuri kati ya taasisi za umma. Kwa niaba ya wagonjwa na wateja wetu, tunasema asanteni sana kwa zawadi hizi ambazo zitawasaidia walengwa kwa kiwango kikubwa,” alisema Mwashtete.

Ameongeza kuwa msaada huo umewatia moyo watumishi wa afya na kuonyesha namna taasisi za umma zinavyoweza kushirikiana kwa manufaa ya wananchi.

“Tunathamini sana mchango huu, kwani unaonyesha dhamira njema ya Serikali kupitia Shirika la Posta katika kusaidia jamii na kuboresha huduma za afya,” alimalizia.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VIONGOZI WA BARAZA KUU LA WAISLAMU BAKWATA MKOA WA MBEYA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU JIJINI MBEYA.

November 9, 2025

TUME YATANGAZA WABUNGE 115 WA VITI MAALUM

November 7, 2025

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025224

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025213

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024197

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025126
Don't Miss

Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Tumbo Kila Siku Bila Kujua Chanzo

By Mbeya YetuNovember 10, 20250

Kwa muda wa takriban miaka miwili, nilikuwa nikiamka kila siku na maumivu makali ya tumbo.…

Nilivyolipa Madeni Yote na Kuanzisha Biashara Mpya Bila Kukopa Popote

November 10, 2025

Nilivyofanikiwa Kumaliza Migogoro Kati ya Watoto Wangu na Kurudisha Upendo Nyumbani

November 9, 2025

Nilivyopata Kazi Ndoto Zangu Baada ya Kuacha Kusema “Sina Bahati” Kila Wakati

November 9, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilivyopata Nafuu Baada ya Kuugua Tumbo Kila Siku Bila Kujua Chanzo

November 10, 2025

Nilivyolipa Madeni Yote na Kuanzisha Biashara Mpya Bila Kukopa Popote

November 10, 2025

Nilivyofanikiwa Kumaliza Migogoro Kati ya Watoto Wangu na Kurudisha Upendo Nyumbani

November 9, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025224

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025213

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024197
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.