Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo

February 8, 2026

TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya

February 8, 2026

New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama

February 8, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo
  • TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya
  • New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama
  • Utengule Usangu Yapata Jezi, Majiko ya Gesi na Msaada wa Kijamii Kutoka kwa Mbunge Ndingo
  • Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya
  • Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H
  • Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee
  • Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania
Habari za Kitaifa

RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania

Mbeya YetuBy Mbeya YetuOctober 18, 2025Updated:October 18, 2025No Comments11 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwathamini zaidi wataalamu wa afya wanaohudumia watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda wao (njiti), kutokana na mazingira magumu na changamoto wanazokabiliana nazo katika utoaji wa huduma hizo.

Malisa aliyasema hayo Oktoba 17, 2025, wakati wa ufunguzi wa ukarabati wa wodi ya watoto wachanga (Neonatal Care Unit – NCU) katika Hospitali ya Wazazi Meta, ukarabati uliotekelezwa na Taasisi ya Afya Ifakara (Ifakara Health Institute – IHI) kwa ushirikiano na wadau wa NEST360 Tanzania.

“Kwa wachache tuliobahatika kuona hali ya wodi hii, imenijengea hofu na kunifanya nione thamani ya maisha kwa undani zaidi. Tunapaswa kuwathamini wataalamu hawa kwa moyo mkubwa, kwani wanahudumia watoto katika mazingira magumu yanayohitaji upendo na uvumilivu mkubwa,” alisema Malisa.

Akiipongeza Taasisi ya Ifakara na wadau wa NEST360 kwa juhudi za kuboresha miundombinu ya afya, Malisa alisisitiza kuwa vifaa vilivyotolewa vitumike ipasavyo kwa manufaa ya Watanzania, hususan wananchi wa Mkoa wa Mbeya.

“Nawashukuru wadau wetu kwa uzalendo wao. Serikali ya Awamu ya Sita imeweka msingi imara wa miundombinu ya afya, na juhudi hizi za wadau ni mwendelezo wa jitihada hizo. Nikiwa Mkuu wa Mkoa, nitaendelea kushiriki kwa vitendo — kila mwaka nitanunua kitanda kimoja kwa ajili ya watoto njiti chenye thamani ya Sh12 milioni,” alisema.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wadau wengine kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya afya, hasa kwenye wilaya tano za Mkoa wa Mbeya, ili kuhakikisha miundombinu ya hospitali inaimarishwa na maisha ya watoto wachanga yanaokolewa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Ifakara, Dkt. Honorant Masanja, alisema mpango wa NEST360 ulianza kutekelezwa mwaka 2019 hadi 2023 katika awamu ya kwanza, ukiwahusisha hospitali saba ikiwemo Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

“Kuanzia mwaka 2024 tumeanza awamu ya pili ya mpango huu, ambapo Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Mbeya na Makandana zimeongezwa. Awamu hii inatarajiwa kukamilika mwaka 2028,” alisema Dk. Masanja.

Amefafanua kuwa mpango huo unalenga kuunga mkono juhudi za serikali kupunguza vifo vya watoto wachanga, ambapo kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, mtoto mmoja hufariki kila baada ya dakika 10 nchini.

“Asilimia 80 ya vifo hivi vinaweza kuzuilika endapo kutakuwepo na wahudumu wa afya wenye ujuzi wa kutosha, vifaa tiba vya kisasa na mazingira rafiki ya utoaji huduma,” aliongeza.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dkt. Godlove Mbwanji, alisema serikali imefanya kazi kubwa kuboresha sekta ya afya, lakini bado inahitaji ushirikiano wa wadau.

“Tumeona hali halisi kwenye wodi hii ya watoto wachanga — inahitaji uwekezaji mkubwa katika vifaa, rasilimali watu na miundombinu. Ni lazima taasisi binafsi na wananchi wajitokeze kusaidia, kwani hawa watoto wadogo ndiyo taifa la kesho,” alisema Dkt. Mbwanji.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya

January 31, 2026

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAFUNGUA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 KWA MATEMBEZI YA AMANI – MBEYA MJINI

January 30, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025333

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025139
Don't Miss
Video Mpya

Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo

By Mbeya YetuFebruary 8, 20263

TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya

February 8, 2026

New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama

February 8, 2026

Utengule Usangu Yapata Jezi, Majiko ya Gesi na Msaada wa Kijamii Kutoka kwa Mbunge Ndingo

February 7, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo

February 8, 2026

TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya

February 8, 2026

New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama

February 8, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025333

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.