Wanachama wa CCM kutoka Mbeya Mjini na Vijijini wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kumlaki Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitokea mkoani Rukwa kuelekea Dar es Salaam.
Wanachama hao walikaa uwanjani tangu saa 1 asubuhi hadi jioni wakisubiri kwa hamasa kumuona kiongozi wao, wakisema wanavutiwa na siasa za hekima, upendo na maendeleo za Dkt. Samia.

