Diwani wa Kata ya Ilomba, Ndg. Noah Edson Mwakisu, leo amerejesha fomu za kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya kupitia CCM. Akizungumza katika Ofisi za CCM Mbeya Mjini, Mwakisu alisema anagombea nafasi hiyo ili kulipa jiji mwelekeo mpya wa maendeleo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wenye maono, ushirikiano na uwajibikaji.
Mwakisu alisema Mbeya ina fursa kubwa za kimaendeleo kutokana na mazingira na jiografia yake, hivyo inahitaji kiongozi anayeendana na mahitaji ya kizazi cha sasa, hususan vijana ambao ndio nguvu ya uchumi wa jiji. Aliomba sapoti na baraka za wananchi, akiahidi kulifanya jiji hilo mfano wa kuigwa endapo atapewa dhamana.
Kurejesha fomu hizo kunamweka rasmi katika kinyang’anyiro cha ndani ya CCM cha kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya mwaka huu.
Trending
- MAZISHI YA SAMSON MWAMAKIMBULA
- Mbinu aliyotumia kupata kazi ya udereva baada ya kusota sana
- MHE. SALOME MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI
- Hofu yake zilianza kuathiri hata furaha ya ndoa yake
- MASACHE AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUSHIKILIA AMANI
- MH. MASACHE: TUENDELEE KUISIMAMIA MIRADI ILIYOKUWEPO NA KUIBUA MIPYA AWASHUKURU WANA CHUNYA
- MH. NOAH MWAKISU AAPISHWA RASMI KUWA DIWANI KATA YA ILOMBA
- Dourmohamed Issa ashinda kwa kishindo Umeya na kutetea nafasi yake

