Maafisa Usafirishaji maarufu kama Bodaboda Mkoani Iringa wamelaani kitendo cha baadhi ya vijana kukubali kushawika na kushiriki kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha kwamba ni maandamano ya amani.
Kauli hiyo imetolewa Desemba 11, 2025 na kundi hilo la vijana ambapo wameonyesha kutofurahishwa na vitendo viovu ikiwemo uchomaji wa miundombinu mbalimbali jambo ambalo linapelekea kudhorota kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

