Haikuanza kwa kishindo, bali kwa kupotea taratibu. Kwanza ilikuwa kazi. Niliitwa ofisini na kuambiwa huduma zangu hazihitajiki tena. Hakukuwa na kosa kubwa wala onyo la mapema. Niliondoka nikiwa na maswali mengi kuliko majibu. Nilijifariji kuwa nitaanza upya, bado nina nguvu, bado nina ndoto.
Lakini pigo la pili lilikuwa biashara. Ile niliyokuwa nimeijenga kwa miaka ilianza kudorora bila sababu. Wateja walipungua, bidhaa zilikaa, madeni yakaanza kunivuta chini. Nilijaribu mikakati mipya, nikapunguza gharama, nikafanya kila nilichojua lakini hali ilizidi kuwa mbaya.
Ilionekana kama mkosi ulikuwa umenikalia.
Marafiki nao walianza kupotea. Simu zangu hazikupokelewa, mipango ilivunjwa, na nilijikuta peke yangu. Wale niliowasaidia awali hawakuonekana. Nilihisi kudharauliwa na kusahauliwa. Soma zaidi hapa

