Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya

February 16, 2026

TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA

February 16, 2026

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya
  • TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA
  • AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
  • SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN
  • EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50
  • Kanisa la Moravian Tanzania Lamkabidhi Yona Sonelo Tuzo Maalum Baada ya Shahada ya Heshima Australia
  • Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji
  • RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MAHUNDI: SERIKALI YAELEZA SABABU ZA KUTOWALAZIMISHA WATOTO KUWAHUDUMIA WAZAZI.
Habari za Kitaifa

MAHUNDI: SERIKALI YAELEZA SABABU ZA KUTOWALAZIMISHA WATOTO KUWAHUDUMIA WAZAZI.

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJanuary 28, 2026No Comments23 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Serikali imesema haina haja ya kuweka sharti la kisheria linalowalazimisha watoto kuwahudumia wazazi wao wasiojiweza, ikieleza kuwa suala hilo tayari linashughulikiwa kupitia misingi ya kifamilia na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa kinondoni Mhe. Tarimba Gulam Abbas lililohoji “Je Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kutunza wazazi wao wasiojiweza”?

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali inatambua umuhimu wa familia na jamii katika kuchukua jukumu la kulea na kuwahudumia wazee, akisisitiza kuwa huo ni msingi wa mila na desturi za Watanzania.

Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma na matunzo kwa wazee kupitia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, Toleo la mwaka 2024, ambayo inasisitiza wajibu wa familia na jamii katika kuwahudumia wazee wao.

“Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa familia na jamii katika kuchukua jukumu la kulea na kutunza wazee, kwani huu ndio msingi wa mila na desturi za Kitanzania na nguzo muhimu katika kujenga mshikamano wa kijamii. Katika kuimarisha huduma na matunzo kwa wazee, Serikali imefanikiwa kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na kuandaa toleo la mwaka 2024, ambalo linaeleza bayana wajibu wa familia na jamii katika kusimamia matunzo ya wazazi na wazee kwa ujumla, Sera hiyo pia imeweka msisitizo wa kuimarisha mifumo ya kisheria utakaolinda na kuendeleza ustawi wa wazee pamoja na watoto wanaowatunza. Kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kutoa maoni juu ya masuala muhimu ya kuzingatiwa katika sheria hiyo.”amesema Mhe. Mahundi

Hata hivyo, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha maadili ya uwajibikaji wa kifamilia na kuimarisha mifumo ya kijamii inayosaidia ustawi wa wazee nchini.

Na Jackline Minja MJJWM-Dodoma

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

February 14, 2026

KUMBUKUMBU YA EDWARD NGOYAI LOWASSA

February 10, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025347

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024231

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025140
Don't Miss
Video Mpya

Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya

By Mbeya YetuFebruary 16, 20265

ZAIDI ya kaya 200 zimepata madhara ya kukosa makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa na nyingine kubomoka kufuatia mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali zinazoendelea kunyesha katika Nyanda za Juu Kusini.

Mbali na makazi kuharibika, vyakula na mavazi pia vimeathirika baada ya maji kujaa kwenye nyumba na mali nyingi kufunikwa na tope.

Uharibifu huo umeripotiwa katika kata sita, ambazo ni Iganzo, Isanga, Karobe, Iyunga, Nzovwe na Iwambi, wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, aliyefika kujionea hali halisi ya wananchi walioathirika.

Baadhi ya wakazi wamesema chanzo kikubwa cha mafuriko hayo ni mifereji kuziba, hali iliyosababisha maji kuingia moja kwa moja kwenye makazi yao.

Licha ya uharibifu mkubwa wa mali na makazi, hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa hadi sasa.

TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA

February 16, 2026

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026

SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

February 15, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya

February 16, 2026

TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA

February 16, 2026

AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI

February 15, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025347

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024231
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.