Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Salim Abri Asas, ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Soko la Matola jijini Mbeya, akieleza kuwa haiwezekani kukamilika mwezi Mei kama ilivyopangwa.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi katika maadhimisho ya miaka 49 ya CCM, Asas alisema mradi unasuasua licha ya fedha kuwepo. Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dk. Mohamed Issa, alimweleza kuwa mkandarasi ameshindwa kusimamia fedha za mradi ipasavyo.
Kwa upande wake, MNEC Ndg. Ndele Mwaselela alisema idadi ndogo ya wafanyakazi na kasi ndogo ya ujenzi ni sababu kuu zinazoathiri ukamilishaji wa mradi.
Ndg. Asas alisema atawasilisha taarifa ya kweli kwa mamlaka husika, akisisitiza kuwa hatakubali kutoa taarifa ya kukamilika kwa mradi wakati hali halisi ni tofauti.
Trending
- Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya
- TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA
- AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
- SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN
- EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50
- Kanisa la Moravian Tanzania Lamkabidhi Yona Sonelo Tuzo Maalum Baada ya Shahada ya Heshima Australia
- Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji
- RC Malisa Afungua Mafunzo ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mbeya

