Mtu anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya, Tido Kadaga (20), amekutwa amefariki dunia baada ya mwili wake kuonekana ukielea kwenye dimbwi la maji katika Mtaa wa Maili Tano, Kata ya Iganzo, Jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, walipokea taarifa kutoka kwa mashuhuda kuhusu mwili unaoelea majini na kufika eneo la tukio, kisha kuuopoa na kuupeleka Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa uchunguzi zaidi.
Mrakibu Mwandamizi wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya, Malumbo Ngata, amesema tukio hilo liliripotiwa majira ya mchana na baada ya uchunguzi wa awali kubainika marehemu ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza CBE.
Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Dk Beny Mwenda, amesema wanangoja taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania kabla ya kutoa ufafanuzi zaidi.
Trending
- “Ndingo: Uongozi wa Samia Ni Ukombozi Mkubwa kwa Wanawake Tanzania.”
- WADAU WATAKIWA KUUNGA MKONO MALEZI YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM
- Mwalunenge Achangia Milioni 3 Baada ya Wanawake MZRH Kutoa Mashine ya EEG
- Comfy Mum na TNCC Wawafariji Wakinamama Wodi ya Wanawake Hospitali ya Sinza
- Mbunge CCM,wapinzani waimarisha umoja,wajadili maendeleo ya wana Mbeya
- Dkt. Tulia Aunga Mkono Ujenzi wa Barabara Bombambili kwa Mifuko 100 ya Saruji na tripu 10 za mawe
- SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA AMBAYE ANGEKUWA HAI JANA ANGETIMIZA UMRI WA MIAKA 100
- Mwalupindi Akabidhi Tuzo Vitabu na kufuturisha wanafunzi Kuimarisha Elimu Sangu Sekondari

