MRADI WA REGROW KUCHOCHEA UCHUMI WA WANANCHI WANAOPAKANA NA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA
Wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Nyererevinanufaika na Mradi wa REGROW unaotekelezwa nchinikupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.
Hayo yamesemwa Jijini Mbeya na Bi. Blanka Aquilinus Tengia Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TANAPA, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na Bodi ya Bonge la Maji Rufiji (RBWB).Lengo la mradi ni kuboresha usimamizi wa maliasili sanjari na kukuza utalii Kusini mwa Tanzania.
Blanka Tengia amesema mradi ulianza mwaka 2017 baada ya tafiti mbalimbali kufanyika na ni wa thamani ya Dola za marekani milioni 150 sawa na takribani shilingi za kitanzania bilioni 345.
Aidha, moja ya shughuli zinazotekelezwa ni kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na majengo ndani ya hifadhi nne za kipaumbele. na miundombinu ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Mbali ya kuboresha miundombinu Mradi wa REGROW unachochea ukuaji wa wa wananchi kiuchumi hususani wanaoishi nyirani na hifadhi zilizotajwakwa kusaidia uanzishwaji wa miradimiradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi, ufadhili wa masomo kwa vijana, vikundi kupewa mtaji wa kukopeshana kwa riba nafuu na kuiwezesha jamii kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu. Pia mradi unatekeleza shughuli za utunzaji wa vyanzo vya maji kwenye eneo la juu la Hifadhi ya Taifa Ruaha ambavyo ni vyanzo vya maji kwa mto Ruaha Mkuu.
Katika hatua nyingine Blanka amesihi wananchi wanaoishi pembezeno mwa hifadhi kuzipenda na kuzitunza hifadhi hizo na kufanya Utalii wa ndani ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kukuza Utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.
Trending
- Dkt. Tulia Ackson Ahutubia Jukwaa la Kibunge la G20, Asisitiza Umuhimu wa Usawa wa Kijinsia
- OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAZINDUA PROGRAMU YA UJASIRIAMALI WA MAZINGIRA
- MZRH Wananchi Wote Mnakaribishwa katika Bonanza Jumamosi 9/11/2024
- Polisi Mbeya Wakamata Watuhumiwa 176 Katika Operesheni ya Kuimarisha Usalama
- Tiba ya kweli ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB)
- MASHEIKH WATOA UJUMBE MAALUMU KWA VIJANA SHEREHE ZA MAULID MASJID TAWFIQ BLOCK ‘Q’ SOWETO MBEYA
- MAKALA: MAHAFALI YA 22 TAASISI YA UHASIBU TANZANIA TIA KAMPASI YA MBEYA WAHITIMU WABUNIFU WAZAWADIWA
- Fanya hivi ukutane na muujiza wa kupata kazi au ajira kwa wepesi!