Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea ametoa wito kwa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za rufaa za mikoa Tanzania Bara kwenda kuongeza Ubunifu wa kuanzisha huduma mpya za Kibingwa katika hospitali zao ili wananchi wapate huduma bora za Afya Dkt Nyembea ametoa wito huo leo tarehe 20 Septemba, 2024 jijini Mbeya katika kuhitimisha kikao kazi cha Waganga Wafawidhi, Wauguzi Wafawidhi, Makatibu wa Hospitali na Waratibu wa Ubora wa Huduma(QI) wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Tanzania bara.“Niwaelekeze Kupitia kikao hiki kahakikisheni mnakwenda kuboresha huduma kwa kuanzisha angalau huduma mpya za kubingwa nane katika Hospitali zenu ili kuendelea kuongeza imani kwa wananchi.”Pia Dkt. Nyembea amewataka wafawidhi kuboresheni stahiki za madaktari Bingwa ili kuwezesha madaktari hao wasifikiri kuhama (retantion) kwa kuwawekea mazingira wezeshi yatakayonfanya Daktari Bingwa abaki kwenye Kituo chako, na kuwashirikisha katika mipango ili nao waweze kuchangia katika kuboresha huduma za kibingwa katika Hospitali zetu.“Kama wizara tumejiwekea malengo kuwa itakapofikia mwaka 2026 huduma nane za kibingwa katika hospitali zote za rufaa za mikoa ikiwemo huduma za utengemao ambapo ni hospitali Saba mpka sasa ambazo zinatoa huduma za utengema.”Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi Dkt. Bahati Msaki ambae ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekotoure amewashukuru viongozi wa Wizara ya Afya kwa kufanikisha kikao hicho kwani kimekuwa kikao kizuri kwa kujitathimini kuona changamoto zilizopo na namna ya kuzikabili na kuwaahidi viongozi hao kwenda kuboresha katika Hospitali zao.”
Trending
- NAIBU WAZIRI MAHUNDI AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA
- MRADI WA REGROW KUCHOCHEA UCHUMI WA WANANCHI WANAOPAKANA NA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA.
- DC. MALISA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA
- Wiki ya huduma kwa Mteja, Mbeya UWSA kituo cha kuchotea maji wananchi Soko Matola chazinduliwa
- WASIOJULIKANA WABOMOA SHULE.
- MZRH YAENDELEA KUWA KITUO CHA MFANO KATIKA USIMAMIZI WA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
- SENETI MKOA WA WA MBEYA WAMUOMBA MWENYEKIT KUWASIMAMIA MIKOPO INAYOTOLEWA NA JIJI
- Mbeya UWSA yaadhimisha wiki ya mteja kwa kuwapongeza Mawakala wake