Sharif Abdul Afisa Mwandamizi kitengo cha mahusiano Jamii na ujirani mwema hifadhi ya Taifa Ruaha amesema kupitia mradi wa REGROW wameandaa Muongozo rafiki wa kupokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi.
Amesema kupitia mradi wa REGROW viongozi na kamati za kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka mkoa wamejengewa uwezo kwa kupewa elimu namna ya kutumia muongozo huo ili kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi. Lengo nikuhakikisha wananchi wanaoathirika na shughuli za hifadhi au Mradi wa REGROW wanawasilisha malalamiko yao na yanashughulikiwa kwa utaratibu unaofahamika.
Aidha Abdul amewasihi wananchi wenye malalamiko wafike ofisi za Serikali ya Kijiji nakuwasilisha malalamiko yao au wapige simu ya bure moja kwa moja kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha namba 0800110801 na Wizara ya Maliasili na Utalii namba 0800110804 endapo lalamiko linahusu Hifadhi au Mradi wa REGROW. Malalamiko yote yatashughulikiwa kwa usiri na mlalamikaji atalindwa na sheria na tararibu za nchi.
Trending
- NAIBU WAZIRI MAHUNDI AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA
- MRADI WA REGROW KUCHOCHEA UCHUMI WA WANANCHI WANAOPAKANA NA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA.
- DC. MALISA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA
- Wiki ya huduma kwa Mteja, Mbeya UWSA kituo cha kuchotea maji wananchi Soko Matola chazinduliwa
- WASIOJULIKANA WABOMOA SHULE.
- MZRH YAENDELEA KUWA KITUO CHA MFANO KATIKA USIMAMIZI WA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
- SENETI MKOA WA WA MBEYA WAMUOMBA MWENYEKIT KUWASIMAMIA MIKOPO INAYOTOLEWA NA JIJI
- Mbeya UWSA yaadhimisha wiki ya mteja kwa kuwapongeza Mawakala wake