Kaimu Mtendaji Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya Mhandisi Barnabas Konga katika maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza machi 16,2024 ameendelea kutolea taarifa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka taarifa iliyoambatana na ziara ya kuitembelea miradi hiyo ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu shilingi bilioni 250 unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji ambapo Kampuni ya China Railway Connstuction ndiyo imepewa kandarasi chini ya Mhandisi Mshauri Kampuni ya GKW Consultant awamu ya kwanza zitatumika shilingi bilioni 119.
Konga amesema Jiji la Mbeya na Mbalizi lina vyanzo ishirini ambavyo vinazalisha lita milioni 66.5 kwa siku wakati uhitaji ni lita milioni 90 kwa siku.
Mhandisi Barnabas Konga katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan wametekeleza miradi mbalmbali kwa gharama ya shilingi bilioni kumi.
Mhandisi Mkazi wa mradi wa Kiwira Audax Rweyemamu amesema mradi umeanza kutekelezwa mwezi April 2023 na utakamilika kwa kipindi cha miezi 24 mwaka 2025 utakuwa unatoa maji.
Ujenzi umefikia asilimia kumi mpaka sasa na utazalisha lita milioni 117 kwa siku ambapo unakuwa na sehemu ya kutibu maji pia matanki makubwa mawili eneo la Sistila na Forest Mpya.
Kaimu Mtendaji Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya Mhandisi Barnabas Konga katika maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza machi 16,2024 ameendelea kutolea taarifa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka taarifa iliyoambatana na ziara ya kuitembelea miradi hiyo ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu shilingi bilioni 250 unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji ambapo Kampuni ya China Railway Connstuction ndiyo imepewa kandarasi chini ya Mhandisi Mshauri Kampuni ya GKW Consultant awamu ya kwanza zitatumika shilingi bilioni 119.
Konga amesema Jiji la Mbeya na Mbalizi lina vyanzo ishirini ambavyo vinazalisha lita milioni 66.5 kwa siku wakati uhitaji ni lita milioni 90 kwa siku.
Mhandisi Barnabas Konga katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan wametekeleza miradi mbalmbali kwa gharama ya shilingi bilioni kumi.
Baadhi ya miradi ni pamoja na mradi wa Mwaashali uliogharimu shilingi milioni 400 unazalisha lita milioni moja kwa siku,mradi wa Nzovwe Isyesye umegharimu shilingi milioni 930 unaozalisha lita milioni nne kwa siku,mradi wa UVIKO unazalisha lita milioni kwa siku,Mwasenkwa Itagano wenye thamani ya shilingi bilioni 5.2 unazalisha lita milioni 2.6,mradi wa Ilunga unazalisha lita milioni kumi.
Kwa upande wake Mhandisi Mkazi wa mradi wa Kiwira Audax Rweyemamu amesema mradi umeanza kutekelezwa mwezi April 2023 na utakamilika kwa kipindi cha miezi 24 mwaka 2025 utakuwa unatoa maji.