Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Tazama muonekano mpya wa Soko la Kariakoo
- TGNP na CARE Waimarisha Elimu ya Tabia Nchi Mbeya
- New Asante Mbeya Yapongeza TAKUKURU Mbeya kwa Elimu ya Uadilifu na Kufungua Uelewa wa Wanachama
- Utengule Usangu Yapata Jezi, Majiko ya Gesi na Msaada wa Kijamii Kutoka kwa Mbunge Ndingo
- Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya
- Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H
- Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee
- Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei
Author: Mbeya Yetu
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la CARE wametoa mafunzo kwa wawezeshaji wa ngazi ya jamii kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mkoani Mbeya kupitia Mradi wa Ustahimilivu Wake, Dunia Yetu unaotekelezwa katika vijiji 300 vya Mbeya, Njombe na Iringa.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika kijiji cha Chimala, wilayani Mbarali, yakilenga kuwajengea wakulima na wafugaji uelewa wa masuala ya jinsia, utunzaji wa mazingira na mbinu za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Bahati Ndingo, amegawa jezi, sufuria, majiko ya gesi pamoja na sabuni kwa wananchi na vikundi mbalimbali vya vijana katika Kata ya Utengule Usangu, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.
Msaada huo umetolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika kiwilaya, yakilenga kuimarisha michezo, matumizi ya nishati safi na ustawi wa jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Ndingo amesisitiza umuhimu wa vijana kukuza vipaji vyao, akibainisha kuwa michezo, hususan soka, ni ajira. Aidha, ametangaza mpango wa kuanzisha mashindano ya soka yajulikanayo kama “Bahati Ndingo Cup” baada ya msimu wa mavuno.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Health Service Tanzania zimeingia katika makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania. Akizungumza jijini Mbeya, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, alisema ushirikiano huo utawezesha kubadilishana ujuzi na uzoefu kati ya sekta ya umma na binafsi kwa manufaa ya wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Aga Khan Health Service Tanzania, Sisawo Konteh, alisema makubaliano hayo yataimarisha huduma za kliniki, kujenga uwezo wa watumishi, kuboresha mifumo ya ubora na kusaidia hospitali hiyo kupata ithibati. Ushirikiano huo pia utahusisha mafunzo, tafiti na kuendeleza huduma bingwa ikiwemo saratani na magonjwa ya moyo, pamoja na kukuza utalii wa tiba katika mkoa wa Mbeya.
Diwani wa Kata ya Utengule Usangu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Ismail Matipa, ametoa sare za shule kwa wanafunzi 400 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza, katika Shule ya Sekondari Utengule Usangu.
Hatua hiyo imelenga kuondoa changamoto ya baadhi ya wazazi kuchelewesha au kushindwa kuwapeleka watoto wao shule pindi msimu wa masomo unapoanza, hali inayosababishwa na ukosefu wa sare za shule.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Diwani Matipa amesema utoaji wa sare hizo ni sehemu ya jitihada zake za kuunga mkono elimu na kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza masomo kwa wakati bila vikwazo vya kiuchumi.
Ameeleza kuwa tukio hilo limefanyika katika wiki ya maadhimisho ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimiza miaka 49 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977, ikiwa ni ishara ya kuenzi mchango wa chama hicho katika maendeleo ya elimu na ustawi wa jamii.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Salim Abri Asas, ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Soko la Matola jijini Mbeya, akieleza kuwa haiwezekani kukamilika mwezi Mei kama ilivyopangwa.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi katika maadhimisho ya miaka 49 ya CCM, Asas alisema mradi unasuasua licha ya fedha kuwepo. Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dk. Mohamed Issa, alimweleza kuwa mkandarasi ameshindwa kusimamia fedha za mradi ipasavyo.
Kwa upande wake, MNEC Ndg. Ndele Mwaselela alisema idadi ndogo ya wafanyakazi na kasi ndogo ya ujenzi ni sababu kuu zinazoathiri ukamilishaji wa mradi.
Ndg. Asas alisema atawasilisha taarifa ya kweli kwa mamlaka husika, akisisitiza kuwa hatakubali kutoa taarifa ya kukamilika kwa mradi wakati hali halisi ni tofauti.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ameshiriki Mkutano wa 67 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi 9 wanachama za Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) unaofanyika Ezulwini, Ufalme wa Eswatini tarehe 2-3 Februari, 2026. Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo umejadili mikakati ya kuimarisha mifumo ya afya ya nchi wanachama wa ECSA-HC, hususan kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani kote yaliyopelekea kupungua au kusitishwa kabisa kwa upatikanaji wa fedha za kufadhili miradi ya afya kutoka kwa wafadhili waliozoeleka.…
