Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Wizara ya Mawasiliano Yaendelea Kushirikiana kwa Karibu na Jeshi la Polisi Kukabili Utapeli Mtandaoni – Mhandisi Maryprisca Mahundi

May 12, 2025

TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025

May 12, 2025

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Wizara ya Mawasiliano Yaendelea Kushirikiana kwa Karibu na Jeshi la Polisi Kukabili Utapeli Mtandaoni – Mhandisi Maryprisca Mahundi
  • TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025
  • UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA
  • MBEYA CITY YARUDI NBC PREMIER LEAGUE KIBABE FURAHA YAREJEA KWA WAKAZI JIJINI MBEYA
  • Mh. Mahundi Atoa Wito kwa Wasichana wa Mzumbe Ndaki ya Mbeya Kujikita Katika Masomo na Maadili
  • WANANCHI:”DKT TULIA AMEGUSA MAKUNDI YOTE MBEYA YUPO YUPO SANA”
  • WASANII BONGO MOVIE WAMUELEZEA DKT TULIA WALIPOSHIRIKI TULIA MARATHON MBEYA
  • WANAMWEF WALIVYOSHIRIKI TULIA MARATHON
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA
Habari za Kitaifa

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMay 12, 2025Updated:May 12, 2025No Comments43 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo Mei 12, 2025 ambapo Tume imetangaza kugawanywa kwa majimbo na kubadilisha majimbo.

 

 

Na. Mwandishi Wetu, Dodoma

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini. 

Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024. 

Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Kivule amabalo limegawanywa kutoka Jimbo la Ukonga na  Jimbo la Uchaguzi la Chamanzi  ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala yote ya mkoani Dar es Salaam.

“Mkoani Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba na Mkoani Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Mbeya Mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Uyole,” amesema.

Ameongeza kuwa Mkoani Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la uchaguzi la Bariadi Mjini.

Jaji Mwambegele amesema Mkoani Geita yameanzishwa majimbo mawili ambapo Jimbo la Uchaguzi la Busanda limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Katoro na Jimbo la Uchaguzi la Chato limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Chato Kusini.

“Mkoani Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Itwangi,” amesema.

Akizungumza kuhusu majimbo kumi na mbili (12) ya uchaguzi yaliyobadilishwa majina, Jaji Mwambegele ameyataja majimbo hayo kuwa ni pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Chato ambalo limebadilishwa jina kuwa Jimbo la Uchaguzi la Chato Kaskazini. 

“Jimbo la Uchaguzi la Nkenge limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Missenyi, Jimbo la Uchaguzi la Mpanda Vijijini limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Tanganyika na Jimbo la Uchaguzi la Buyungu limebadilishwa jina sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Kakonko,” amesema. 

Ameongeza kuwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi Vijijini, Jimbo la Uchaguzi la Manyoni Mashariki limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Manyoni na Jimbo la Uchaguzi la Singida Kaskazini limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Ilongero.

Majimbo mengine ni Jimbo la Manyoni Magharibi kuwa Jimbo la Itigi, Jimbo la Singida Mashariki kuwa Jimbo la Ikungi Mashariki, Jimbo la Singida Magharibi kuwa Jimbo la Ikungi Magharibi, Jimbo la Tabora Kaskazini kuwa Jimbo la Uyui na Jimbo la Handeni Vijijini kuwa Jimbo la Handeni.

“Kutokana na ongezeko hilo la majimbo nane, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano.  Kati ya majimbo hayo 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa  kutakuwa na kata 3,960 zitakazofanya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Wizara ya Mawasiliano Yaendelea Kushirikiana kwa Karibu na Jeshi la Polisi Kukabili Utapeli Mtandaoni – Mhandisi Maryprisca Mahundi

May 12, 2025

TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025

May 12, 2025

Mashindano ya Riadha ya Betika Mbeya Tulia Marathon 2025 Yametamatika kwa Mafanikio Makubwa

May 10, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024169

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202481

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202457

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MBEYA YAANZA,WANAHABARI WATEMBELEA MIRADI

March 16, 202444
Don't Miss
Habari za Kitaifa

Wizara ya Mawasiliano Yaendelea Kushirikiana kwa Karibu na Jeshi la Polisi Kukabili Utapeli Mtandaoni – Mhandisi Maryprisca Mahundi

By Mbeya YetuMay 12, 20256

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema kuwa Wizara…

TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025

May 12, 2025

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 2025

MBEYA CITY YARUDI NBC PREMIER LEAGUE KIBABE FURAHA YAREJEA KWA WAKAZI JIJINI MBEYA

May 11, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Wizara ya Mawasiliano Yaendelea Kushirikiana kwa Karibu na Jeshi la Polisi Kukabili Utapeli Mtandaoni – Mhandisi Maryprisca Mahundi

May 12, 2025

TIMU YA MADAKTARI NA WAUGUZI KUTOKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, TANZANIA WAMETEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA, TAREHE 12 MEI, 2025

May 12, 2025

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024169

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202481

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202457
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.