Watoa huduma ya Afya ya Mama na mtoto wametakiwa kuwa makini wakati wa utoaji huduma ya uzazi ili mama anapokuwa analeta zawadi ya mtoto duniani hasibaki na changamoto yoyote ya kiafya ikiwemo ugonjwa wa fistula.
Leo Mei 21,2025 Wizara ya Afya Idara ya Mama na Mtoto inakaa Jijini Mbeya pamoja na Wadau kujadili afua muhimu za kuangazia namna bora ya kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa akina mama kuelekea maadhimisho ya siku ya Fistula Duniani itakaoyadhimishwa Kitaifa Mbeya Mei 23, 2025.
Mkurugenzi Hospitali ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekilage wakati wa ufunguzi Kikao Kazi hicho amesema mama hatakiwi kuwa na tatizo lolote mara baada ya kujifungua.
“Tunajua mama anapokuwa anapomleta mtoto duniani hatakiwi kuwa na tatizo lolote na wote tunajua ni muhimu sana huyu mama wa thamani kumlinda dhidi ya fistula ili kuwa na uzazi endelevu katika Taifa letu”, alisema Dkt. Godlove Mkurugenzi Hospitai ya Rufaa Mbeya.
Naye Mratibu wa Afua za Fistula Tanzania Fidea Obimbo ameseama Wiazara ya Afya inachylua hatua muhimu kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa kutoa huduma karibu kwa wananchi akitaja huduma za kibingwa za madaktari wa Dkt Samia kuwa sehemu ya mapambano hayo.
Bi. Fidea ameongeza kuwa maadhimisho haya mwaka huu yanafanyika Mbeya katika hospitali Kitengo cha Huduma ya Mama na mtoto ili kuenzi wakina mama na kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wenye changamoto ya Fistula.
Bi .Ametoa wito kwa wadau wa Afya kujitokeza kwa wingi kutoa michango yao katika mapambano ya Fistula akisema kuwa idadi ya wadau wanotoa huduma katika eneo la ugonjwa huu kuwa bado ni ndogo sana.
Mkurugenzi wa Fistula Foundation Bw. Clement Ndahani akiongea na vyombo vya habari nje kidogo ya mkutano wa wadau amesema ugonjwa wa fistula unakumba wagonjwa wengi wanaotoka katika Kaya Masikini.
Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Fistula Duniani uhadhimishwa kila mwaka na kwa mwaka 2025 yanafanyika Mkoani Mbeya yakiwa na kauli mbiu isemayo