Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

July 10, 2025

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
  • ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA
  • MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI
  • KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO
  • MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI
  • Msimu wa pili wa tamasha la michezo na vipaji MZRH
  • MKULIMA NA MFUGAJI WA MBARALI ATIA TIMU KIPUTE JIMBO LA MBARALI USANGU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE
  • WAKILI MSOMI KAPTENI MSTAAFU SAMBWEE SHITAMBALA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI.
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Habari za Kitaifa

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 10, 2025No Comments20 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu

Serikali imekubali kutoa mafunzo maalum kwa waandishi wa blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, hatua muhimu itakayowajengea uwezo na kuwaandaa kubeba dhamana kubwa ya usambazaji wa habari sahihi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika Mkutamo wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya habari Katika kufanikisha uchaguzi Mkuu 2025.

Katika mkutano huo kipindi cha majadiliano Mwenyekiti wa Chama cha Mabloga Tanzania (TBN), Beda Msimbe, aliomba serikali kuona umuhimu wa kufunza mabloga wengi ambao sio waandishi lakini wanatengeneza maudhui kuwa na weledi kuandika masuala ya siasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, Julai 9, 2025, Bwana Msimbe alisisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo mabloga, akibainisha kuwa, “Wao wanabeba dhamana kubwa kutokana na wingi wao na wanatengeneza maudhui, na wengine si waandishi wa habari.”

Aliongeza kuwa katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia na akili bandia (AI), vyanzo vya habari vinavyotegemewa zaidi si mitandao ya kijamii, bali maandishi yanayopatikana kwenye blogu na tovuti, hivyo kufanya uhitaji wa mafunzo kuwa mkubwa zaidi.

Bwana Msimbe alitumia fursa hiyo kupongeza uamuzi wa kuandaa kikao hicho muhimu cha wadau, akisema kuwa ni hatua inayostahili kuelekea uchaguzi wa haki na uwazi. Licha ya changamoto ya mada nyingi (tisa) kujadiliwa ndani ya siku moja, alipongeza mkutano huo na jinsi ulivyokwenda.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Ndugu Msigwa, aliiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuandaa mafunzo hayo mapema iwezekanavyo.

Kauli hiyo ya serikali imetafsiriwa na wadau mbalimbali kama hatua ya kutambuliwa rasmi kwa mchango wa mabloga katika tasnia ya habari na katika mchakato wa kidemokrasia.

Chama cha Mabloga Tanzania (TBN) kina wanachama zaidi ya 200 waliotawanyika kote nchini na nchi za nje, hivyo mafunzo haya yatakuwa na athari kubwa katika kuhakikisha usambazaji wa habari sahihi, zenye vigezo vya kitaaluma, na zinazozingatia maadili ya uandishi wa habari wakati wa kipindi cha uchaguzi na baadae.

Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko ambaye alitaka vyombo vya habari na vya usalama kuhakikisha Amani na kuvumiliana kuelekea katika uchaguzi huo.

mwisho

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MHASIBU SUA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SAME MASHARIKI

June 28, 2025

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

June 22, 2025

VIJANA CCM MBEYA DC WAJIPANGA KUPIGA KURA OKTOBA 2025.

June 13, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024174

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202483

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202460
Don't Miss

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

By Mbeya YetuJuly 10, 202520

Na Mwandishi Wetu Serikali imekubali kutoa mafunzo maalum kwa waandishi wa blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu…

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025

KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO

July 1, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

July 10, 2025

ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA

July 6, 2025

MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI

July 3, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024174

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202483

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202569
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.