Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Dkt Tulia Ackson, kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ameigusa familia ya Bi. Lusia Kapangala mkazi wa mtaa wa Mwasote kata ya Itezi jijini Mbeya iliyokuwa imekata tamaa ya maisha kutokana na mapito ya kukosa mahitaji muhimu ikiwemo chakula, mavazi na fedha za kusomesha watoto.
Dkt. Tulia hayo tarehe 12 Julai, 2025 ambapo amesema pamoja na kuihudumia familia hiyo mahitaji muhimu, pia amechukua jukumu la kuwasomesha watoto wote wa familia hiyo, akiwemo kijana Nature Nenelo aliyehitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja la kwanza la alama 13 na kushindwa kuanza masomo ya kidato cha tano kutokana na Bibi yake kukosa fedha.
Kwa upande wake, kijana Nature Nenelo ameeleza namna alivyopitia ugumu katika safari yake ya masomo ikiwa ni pamoja na kukata tamaa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano baada ya familia kukosa fedha za kumudu kusomesha watoto wawili, yeye pamoja na kaka yake anayesoma chuo, Huku Bibi yao Bi. Lusia Kapangala akimshukuru Dkt. Tulia pam