Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Naibu Waziri wa Maji Mathew: Aweka Mkazo Kwenye Miradi ya Maji Mbeya na Chunya

December 16, 2025

Hafla ya Makabidhiano ya Vitabu vya Fidia vya Mradi wa Chanzo cha Mto Kiwira

December 15, 2025

WAKUTUBI WAKUTANA MBEYA WAJADILI MFUMO BORA WA MAKTABA NA USOMAJI VITABU KIDIJITALI

December 15, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Naibu Waziri wa Maji Mathew: Aweka Mkazo Kwenye Miradi ya Maji Mbeya na Chunya
  • Hafla ya Makabidhiano ya Vitabu vya Fidia vya Mradi wa Chanzo cha Mto Kiwira
  • WAKUTUBI WAKUTANA MBEYA WAJADILI MFUMO BORA WA MAKTABA NA USOMAJI VITABU KIDIJITALI
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA BENNO MALISA AHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULINDA FEDHA ZA UMMA
  • Suzi alivyomrejesha mpenzi wake na wakafunga ndoa
  • Jinsi unavyoweza kuibadilisha biashara yako na kukupa faida
  • RAIS DKT. SAMIA AKIWASILI SKUA (TANGA) KWA KIKAO CHA NDANI NA VIONGOZI WA JWTZ
  • WAZIRI MKUU- WATANZANIA TUNZENI AKIBA YA CHAKULA▪️Ahimiza matumizi ya mbolea na mbegu za mazao
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA
Habari za Kitaifa

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 2, 2025No Comments13 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email


Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs
Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na Waandishi wa
Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja
kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 02 , 2025.

 

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs
Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na Waandishi wa
Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja
kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 02 , 2025.

 

 

Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima
akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mkutano wa Tume na Waandishi wa
Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja
kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 02 , 2025. 
***************

 

Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kuhamasisha na kuelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba, 2025.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu, uliofanyika tarehe 2 Agosti, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Jaji Mwambegele amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu kwa kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi.
Ameeleza kuwa waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kutumia taaluma yao kuwaelimisha wananchi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ili waweze kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amewakumbusha wanahabari wajibu wao wa kuhakikisha vyama vya siasa na wagombea wanapata nafasi ya kufikisha ujumbe wao kwa wapiga kura katika kipindi cha kampeni.
Aidha, Bw. Kailima amewataka wanahabari kutoa taarifa sahihi kwa umma na kuepuka kusambaza taarifa potofu katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na maadili ya taaluma ya habari.
Amewahimiza waandishi hao kutumia kalamu na nyenzo zao kueneza ujumbe wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ili kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha misingi ya demokrasia.
Pia amewaasa kuepuka kuchapisha au kurusha habari zinazoweza kuwavunja moyo wananchi na kuwafanya waone kama hakuna umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi, iwe ni kama wapiga kura au wagombea.
Mkutano kati ya Tume na Waandishi wa Habari ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya wadau mbalimbali ambayo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikiitisha katika maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mikutano hiyo ilianza tarehe 27 Julai 2025 kwa kukutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa, ikafuatiwa na mkutano na Wawakilishi wa Asasi Zisizo za Kiserikali kisha Wawakilishi wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari.
Mfululizo huu wa mikutano unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 4 Agosti 2025, baada ya mkutano na Waandaji wa Maudhui Mtandaoni, utakaofuatiwa na mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Naibu Waziri wa Maji Mathew: Aweka Mkazo Kwenye Miradi ya Maji Mbeya na Chunya

December 16, 2025

MAHAFALI YA 23 YA TAASISI YA UHASIBU TIA KAMPASI YA MBEYA, RC MALISA AWAALIKA WAWEKEZAJI MKOANI MBEYA.

December 12, 2025

TANZANIA NA MAREKANI ZASONGA MBELE KUKAMILISHA MAKUBALIANO MAKUBWA YA UWEKEZAJI

December 9, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025258

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025235

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024208

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025130
Don't Miss
Habari za Kitaifa

Naibu Waziri wa Maji Mathew: Aweka Mkazo Kwenye Miradi ya Maji Mbeya na Chunya

By Mbeya YetuDecember 16, 202516

Mbeya. Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Eng. Kundo A. Mathew, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miradi…

Hafla ya Makabidhiano ya Vitabu vya Fidia vya Mradi wa Chanzo cha Mto Kiwira

December 15, 2025

WAKUTUBI WAKUTANA MBEYA WAJADILI MFUMO BORA WA MAKTABA NA USOMAJI VITABU KIDIJITALI

December 15, 2025

MKUU WA MKOA WA MBEYA BENNO MALISA AHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULINDA FEDHA ZA UMMA

December 15, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Naibu Waziri wa Maji Mathew: Aweka Mkazo Kwenye Miradi ya Maji Mbeya na Chunya

December 16, 2025

Hafla ya Makabidhiano ya Vitabu vya Fidia vya Mradi wa Chanzo cha Mto Kiwira

December 15, 2025

WAKUTUBI WAKUTANA MBEYA WAJADILI MFUMO BORA WA MAKTABA NA USOMAJI VITABU KIDIJITALI

December 15, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025258

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025235

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024208
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.