Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Aliniahidi ndoa kumbe alikuwa anitumia kimya kimya kuongeza utajiri wake wa kiroho

August 6, 2025

DED MKALAMA ATEMBELEA BANDA LA TARURA MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI-DODOMA

August 6, 2025

“KABLA YA KIPENGA: MASHABIKI WAPAZA SAUTI KWA STARS”

August 6, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Aliniahidi ndoa kumbe alikuwa anitumia kimya kimya kuongeza utajiri wake wa kiroho
  • DED MKALAMA ATEMBELEA BANDA LA TARURA MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI-DODOMA
  • “KABLA YA KIPENGA: MASHABIKI WAPAZA SAUTI KWA STARS”
  • WAKULIMA 18,000 KUNUFAIKA NA KILIMO MISITU – WAZIRI CHANA
  • UJUMBE WA HELEN KELLER WAFIKA KITUO CHA AFYA ISMANI KUJIONEA ZOEZI LA HUDUMA YA UPASUAJI MTOTO WA JICHO
  • Naweza kusema kama sio mtu huyu hadi leo ningekuwa sijaoa!
  • USHIRIKI BENKI NMB MAONESHO KILIMO NANE NANE MBEYA,ELIMU UJASIRIAMALI HUDUMA ZA KIBENKI ZATOLEWA
  • “Rais wa IPU Dkt. Tulia Kuongoza Uzinduzi wa Kitabu cha Ndoto ya Yatima”Mbeya, Septemba 13
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » TCRA Yapaza Sauti Kupitia Kisaka: Bloga Muwe Mabalozi wa Amani Uchaguzi 2025
Habari za Kitaifa

TCRA Yapaza Sauti Kupitia Kisaka: Bloga Muwe Mabalozi wa Amani Uchaguzi 2025

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 4, 2025No Comments7 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu

 Agosti 3, 2025 — Wazalishaji wa maudhui mtandaoni wametakiwa kuepuka kuchapisha taarifa zinazoweza kusababisha taharuki au kuchochea machafuko, hususan katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Kitengo cha Huduma za Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa watoa maudhui mtandaoni ulioandaliwa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Mhandisi Kisaka amesema kuwa kipindi cha uchaguzi huwa na hali ya migawanyiko, mivutano na upotoshaji mkubwa, hivyo ni muhimu mabloga na watoa maudhui wengine kujiepusha kusambaza uvumi, kutangaza kwa umakini, kutopendelea upande wowote na kukemea lugha ya chuki.

“Kama unaona maudhui yanaweza kuleta taharuki ni bora kuachana nayo,” amesema Kisaka.

Ametoa mfano wa machafuko ya uchaguzi yaliyotokea Nigeria mwaka 2011, ambapo watu zaidi ya 800 walipoteza maisha, na Kenya mwaka 2007, ambapo zaidi ya watu 1,000 walifariki huku wengine 600,000 wakikosa makazi.

Ameongeza kuwa vyombo vya habari vinaweza kuwa sehemu ya tatizo endapo vitasambaza uvumi au kuonyesha upendeleo wa kisiasa kwa namna isiyozingatia maadili.

“Uvumi ndiyo chanzo kikuu cha vurugu. Vyombo vya habari vinapaswa kuchunguza uvumi na kutoa taarifa sahihi mapema ili kuzuia machafuko ya kulipiza kisasi,” amesema.

Aidha, Kisaka amewataka mabloga kutochapisha au kurudia vichwa vya habari vyenye lugha ya kichochezi, hata kama kauli hizo zimetolewa na wanasiasa. Amesema lugha ya kudhalilisha inaweza kuchochea ghasia na vitendo vya kikatili.

Pia ametoa angalizo kwa mabloga kuacha matangazo ya moja kwa moja ya kampeni, akieleza kuwa kazi hiyo inapaswa kufanywa na waandishi waandamizi waliobobea katika kuripoti wakati wa migogoro.

“Matangazo ya moja kwa moja ya machafuko yanahitaji uzoefu. ‘One Man Show’ wa bloga hauna nafasi katika mazingira hayo ya shinikizo,” amesema.

Kwa mujibu wa TCRA, mafunzo ya namna ya kuripoti wakati wa maafa na katika mazingira ya uchaguzi ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha uchaguzi wa 2025 unafanyika kwa amani kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

DED MKALAMA ATEMBELEA BANDA LA TARURA MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI-DODOMA

August 6, 2025

UJUMBE WA HELEN KELLER WAFIKA KITUO CHA AFYA ISMANI KUJIONEA ZOEZI LA HUDUMA YA UPASUAJI MTOTO WA JICHO

August 6, 2025

TANZANIA WENYEJI WA WARSHA YA WAKUU WA TAASISI ZA KUPAMBANA NA RUSHWA KUTOKA NCHI ZA SADC

August 4, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024179

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025161

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202581
Don't Miss
Uncategorized

Aliniahidi ndoa kumbe alikuwa anitumia kimya kimya kuongeza utajiri wake wa kiroho

By Mbeya YetuAugust 6, 20251

Kwa kweli mapenzi huwa kipimo cha moyo wa binadamu. Nilipokutana na Joel, nilihisi kama ndoto…

DED MKALAMA ATEMBELEA BANDA LA TARURA MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI-DODOMA

August 6, 2025

“KABLA YA KIPENGA: MASHABIKI WAPAZA SAUTI KWA STARS”

August 6, 2025

WAKULIMA 18,000 KUNUFAIKA NA KILIMO MISITU – WAZIRI CHANA

August 6, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Aliniahidi ndoa kumbe alikuwa anitumia kimya kimya kuongeza utajiri wake wa kiroho

August 6, 2025

DED MKALAMA ATEMBELEA BANDA LA TARURA MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI-DODOMA

August 6, 2025

“KABLA YA KIPENGA: MASHABIKI WAPAZA SAUTI KWA STARS”

August 6, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024179

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025161

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.