Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

March 9, 2026

Uzalendo wa Kweli: King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

March 9, 2026

BAKWATA MBEYA YAANDAA SEMINA ELEKEZI KWA MAIMAMU NA WAHADHIRI JUU YA AMANI

March 9, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.
  • Uzalendo wa Kweli: King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.
  • BAKWATA MBEYA YAANDAA SEMINA ELEKEZI KWA MAIMAMU NA WAHADHIRI JUU YA AMANI
  • MWALUNENGE AHOJI KUFUNGIWA MARA KWA MARA UWANJA WA SOKOINE
  • RAIS Samia Suluhu Hassan ATUMA SALAMU ZA POLE KWA ZAHIR ALLY ZORRO
  • WANAWAKE WATAKIWA KUENDELEA KUPINGA UKATILI KATIKA JAMII
  • Funguka Foundation Yapokea Msaada wa Mashine ya Kufulia Kutoka Wanawake TAKUKURU MBEYA
  • Wanawake TAKUKURU Mbeya Watoa Mashine ya Kufulia kwa Watoto Wenye Mahitaji Maalum
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS
Uncategorized

TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 8, 2025No Comments29 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email




Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akizungumza wakati akitangaza ratiba na orodha ya vyama ambavyo wagombea wake wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watafika katika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma kuchukua fomu za utezi kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Kailima amesema hadi kufikia leo Agosti 08, 2025 vyama 14 vimeijulisha Tume ratiba ya wagombea wa vyama  husika kuchukua  fomu. Zoezi hilo litaanza Agosti 09 hadi 27 mwaka huu na vyama vingine vitakavyojitokeza vitapangiwa  ratiba.
*******
Na Mwandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
(INEC) imetangaza ratiba ya kuchukua fomu za uteuzi kwa wagombea wa vyama 14
vya siasa waliopendekezwa kugombea nafasi za Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaanza kesho tarehe 09 Agosti, 2025.

Mkurugenzi wa INEC, Ndugu,
Kailima Ramadhani akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 08 Agosti, 2025 amewataja
wagombea watakaochukua fomu kesho tarehe 09 Agosti, 2025 kuwa ni kutoka Chama
cha Mapinduzi (CCM), National Reconstruction Alliance (NRA) na Alliance for
African Farmers Party (AAFP).

“Hadi leo tarehe 08 Agosti,
2025, tumepokea barua kutoka katika vyama vya siasa kumi na nne (14) zikiainisha
tarehe na muda ambao wanachama wa vyama vyao waliowapendekeza kugombea nafasi
za Kiti cha Rais na Makamu wa Rais watafika ofisi za Tume zilizopo Njedengwa
Jijini Dodoma kwa ajili ya kuchukua Fomu za Uteuzi,” amesema Ndugu. Kailima.

Amevitaja vyama vingine na
tarehe za wagombea kuchukua fomu kuwa ni pamoja na na Chama cha MAKINI tarehe 10
Agosti, 2025, The National League for Democracy (NLD) tarehe 10 Agosti, 2025,
United Peoples’ Democratic Party (UPDP) tarehe 10 Agosti, 2025 na African
Democratic Alliance Party (ADA – TADEA) tarehe 11 Agosti, 2025.

Vyama vingine ni Union for
Multiparty Democracy (UMD) tarehe 11 Agosti, 2025, Tanzania Labour Party (TLP)
tarehe 11 Agosti, 2025, Chama Cha Kijamii (CCK), tarehe 12 Agosti, 2025, Chama
cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), tarehe 12 Agosti, 2025, Alliance for Democratic
Change (ADC), tarehe 12 Agosti, 2025, Democratic Party (DP) tarehe 13 Agosti,
2025 na National Convention for Construction and Reform (NCCR – MAGEUZI) tarehe
15 Agosti, 2025.

Ndugu Kailima amesema tayari Tume
imeviandikia vyama hivyo vya siasa barua kuvijulisha kuhusu ratiba hiyo ya
utoaji fomu za uteuzi. 


“Aidha, ni muhimu tukumbuke
kuwa, ratiba hii inahusu vyama kumi na nne (14) pekee vilivyowasilisha taarifa
hadi kufikia leo tarehe 08 Agosti, 2025, hivyo iwapo vyama vingine
vitajitokeza, tutaandaa ratiba husika na kuwajulisha,” amesema.

Amevipongeza vyama vyote vya
siasa kwa kuendelea kufanya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na
kuongeza kuwa, Tume kwa upande wake itazingatia katiba, sheria na kanuni wakati
wote wa mchakato wa uchaguzi.
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Funguka Foundation Yapokea Msaada wa Mashine ya Kufulia Kutoka Wanawake TAKUKURU MBEYA

March 8, 2026

Nilipata Miscarriage Mara Tano Hadi Nikapoteza Ndoto Zangu Za Kuwa Mama Mpaka Nilipopata Usaidizi Usio na Madhara

January 25, 2026

Nilifanya Kazi Kwa Miaka Miwili Bila Kupata Promotion Ila Nilijitafutia Hiyo Promotion Mwenyewe

January 25, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025364

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025253

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236

Vijana Wamchana Waziri wa Vijana, ”Si Wananchi, Ila Watumishi Ndio Watakaoniangusha”

December 1, 2025141
Don't Miss
Video Mpya

King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

By Mbeya YetuMarch 9, 20260

Uzalendo wa Kweli: King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

March 9, 2026

BAKWATA MBEYA YAANDAA SEMINA ELEKEZI KWA MAIMAMU NA WAHADHIRI JUU YA AMANI

March 9, 2026

MWALUNENGE AHOJI KUFUNGIWA MARA KWA MARA UWANJA WA SOKOINE

March 9, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

March 9, 2026

Uzalendo wa Kweli: King James Pharmacy Yaweka Alama ya Kipekee MZRH, Yaonyesha Kiu ya Wazawa Kuikwamua Sekta ya Afya.

March 9, 2026

BAKWATA MBEYA YAANDAA SEMINA ELEKEZI KWA MAIMAMU NA WAHADHIRI JUU YA AMANI

March 9, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025364

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025253

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024236
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.