Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini mkoani Mbeya, Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 25 Agosti 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya wananchi wa Jimbo jipya la Uyole katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Dkt. Tulia amechukua fomu hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, huku akipokelewa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na wafuasi wake waliokuwa na shauku kubwa ya kumuona akiendelea kulitumikia Taifa kupitia jimbo hilo jipya.
Aidha, amewataka wananchi wa Uyole kuungana naye katika safari ya maendeleo, akisisitiza kuwa uzoefu wake wa uongozi na nafasi alizowahi kushika kitaifa na kimataifa utakuwa chachu ya kuimarisha ustawi wa wananchi wa jimbo hilo.