Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Sera na Uratibu Zanzibar Hamza Hassan Juma wameimwagia pongezi Benki ya NMB kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali kwa kutoa elimu ya kifedha kwa vijana ili kujikwamua kiuchumi.
Wameyasema hayo walipotembelea Banda la NMB kwenye maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayoendelea viwanja vya Soko la Uhindini jijini Mbeya.
“Mmekuwa na sapoti kubwa kwa serikali kusaidia elimu ya kifedha kwa vijana, Vijana wengi kwa sasa wamejikwamua kiuchumi kutoka na elimu mnayotoa” alisema Waziri Katambi.
Kwa upande wake Waziri Hamza Hassan Juma amesema vijana wengi wa Kizanzibari wamejikita katika ujasiriamali kutoka na elimu kwa vijana inayotolewa na Benki ya NMB.
Akizungumza wakati akiwakaribisha Mawaziri hao, Meneja Mahusiano Mwandamizi wa NMB Josephine Kulwa alisema Benki hiyo imetumia fursa hii ya Wiki ya Vijana kutoa elimu ya kifedha ambako kwa sasa kuna akaunti maalumu inayowagusa bila a wanafunzi wa vyuo vikuu ya Mwanachuo Akaunti.
Amesema akaunti hizi ni rafiki kwa vijana na wanachuo ambapo wakifanya muamala kwa kutumia Mshiko Fasta wanarudishiwa asilimia 30.