Sheikh wa mkoa wa Mbeya Sheikh Msafiri Ayas Njalambaha akiwa na Baadhi Viongozi wa Baraza kuu la Waislamu BAKWATA Mkoa Mbeya walipotembelea mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kiislamu inayojengwa barabara ya Nane Sokomatola Jijini Mbeya.

Miradi huo wa shule ya Sekondari ya Kiislamu unatarajiwa kugharimu kiasi cha Sh Bilioni 4 hadi kukamilika kwake Fedha ambazo zinategemea michango na sadaka za Waislamu na Wadau wa Maendeleo ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya

