Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Mbinu ya kupata faida katika biashara ya samaki, uvuvi

November 21, 2025

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE

November 21, 2025

Mgombea Umeya Jiji la Mbeya, Noah Mwakisu Arejesha Fomu; Aahidi “Ukombozi wa Jiji”

November 21, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Mbinu ya kupata faida katika biashara ya samaki, uvuvi
  • WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE
  • Mgombea Umeya Jiji la Mbeya, Noah Mwakisu Arejesha Fomu; Aahidi “Ukombozi wa Jiji”
  • MVUA ILIYONYESHA LUMBILA IWAMBI MBEYA MITARO YAFURIKA MAKAZI YA WATU YAJAA MAJI BIASHARA ZASIMAMA
  • Afanikiwa kuoa baada ya kuvunja vifungo vya ukoo!
  • MWAKIPESILE: ”YALIYOJIRI OKT 29 YAMETUUMIZA,TUMUUNGE MKONO RAIS,WAZIRI MKUU MWIGULU NI MZALENDO”
  • Hadi nilishindwa kujiamini nikiwa faragha!
  • Rais Samia Ahoji Kilio cha Vijana: “Walikuwa Wanaidai Haki Ipi?”
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE
Habari za Kitaifa

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE

Mbeya YetuBy Mbeya YetuNovember 21, 2025Updated:November 21, 2025No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameelekeza Jeshi la Polisi na Uhamiaji kuhakikisha wanamkamata na kuzuia hati ya kusafiria ya mkandarasi anayejenga mradi wa Kituo cha ukaguzi cha Pamoja kilichopo Muhalala mkoani Singida.

Dkt. Mwigulu amesema kuwa mkandarasi huyo aliaminiwa na Serikali kwa kupewa ujenzi wa mradi huo wa kimkakati uliosimama kwa zaidi ya miaka nane tangu mwaka 2016. Mradi huo unaojengwa na kampuni ya Impresa di Costruzioni Ing. E. Mantovani S.p.A ulipaswa kukamilika mwaka 2018.

Ametoa agizo hilo leo Ijumaa tarehe 21 Novemba, 2025 wakati alipokagua mradi huo katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida ambapo atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa jitihada zimefanyika za kuona mradi huo unaendelea lakini mkandarasi amekuwa akileta ugumu katika utekelezaji “Mkandarasi huyu alitangazwa amefilisika na hawezi kuendelea na mradi na alielekezwa ailipe fidia Tanzania kwasababu ameicheleweshea mradi”

“Naelekeza, Kamishna wa uhamiaji kamata hati yake ya kusafiria, asitoke nje ya nchi mpaka jambo hili liishe, hii ni hujuma ya waziwazi, hii ni dharau ya waziwazi anaifanyia nchi yetu, Jeshi la Polisi mtafuteni mkandarasi huyu popote alipo, tumemuajiri, tunamlipa lakini anajiamulia Kama aendelee na kazi au asiendelee, huyu ni mhalifu akamatwe mpaka jambo hili liishe” amesisitiza Dkt. Mwigulu

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa wakandarasi wa nje wanapaswa kufahamu kuwa wanapokuja kufanya kazi hapa nchini, watambue Tanzania imewaajiri na wasijione kama wao ni mabosi.

“Ninaelekeza wale washirika wetu katika mradi huu, ndani ya mwezi huu jambo hili liwe limekwisha watuambie wanaendelea ama hawaendelei, na Kama hawataendelea Waziri wa Ujenzi uwapatie wakandarasi wadogo wamalizie kazi hii, hii nchi ni yetu na tunawajibu wa kuilinda, na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametuambia hatuna mjomba, tuna mama tu anaitwa Tanzania”

Aidha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameiagiza Wizara ya Ujenzi ihakikishe inausimamia mradi huo ili ukamilike na itumie wakandarasi wazawa , “Ninawahakikishia mradi huu tutaujenga na kuukamilisha”

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amemuagiza Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Abdullah Ulega kuwaelekeza wakandarasi wote kuhakikisha kuwa kila aliyepewa kazi apime kama kazi aliyoifanya inaendana na thamani ya fedha alizopokea.

“Haya ndiyo maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwamba kila mradi, thamani ya fedha iendane na kazi ambayo imeshafanyika, sisi wasaidizi wake tutafuatilia maelekezo haya, hatuwezi ruhusu watu wachezee nchi yetu”

Kadhalika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuilinda Tanzania, ili iendelee kuwa na maendeleo “Mungu ametupa nchi nzuri, nchi hii si mali ya viongozi, nchi hii sio mali ya vyama vya siasa, nchi hii ni yetu sote”

Kwa Upande wake, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema kuwa mradi huo ni mradi wa kielelezo na unafaida nyingi sana ambazo zitalisaidia Taifa ikiwemo kuokoa fedha nyingi zinazowekwa kwenye barabara.

“Vilevile eneo hili litakuwa ni eneo la kibiashara kwasababu watu watapata nafasi ya kufanya biashara na wananchi kutengeneza uchumi wao, sisi Wizara ya ujenzi tupo tayari kujenga ili mradi hui urejee” amesisitiza Waziri Ulega

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VIONGOZI WA BARAZA KUU LA WAISLAMU BAKWATA MKOA WA MBEYA WATEMBELEA MRADI WA UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU JIJINI MBEYA.

November 9, 2025

TUME YATANGAZA WABUNGE 115 WA VITI MAALUM

November 7, 2025

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025228

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025127
Don't Miss
Uncategorized

Mbinu ya kupata faida katika biashara ya samaki, uvuvi

By Mbeya YetuNovember 21, 20250

Kutana na Mgosi kutokea Tanga, kijana ambaye alikuwa akijulikana kama mtu mwenye bidii na moyo…

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE

November 21, 2025

Mgombea Umeya Jiji la Mbeya, Noah Mwakisu Arejesha Fomu; Aahidi “Ukombozi wa Jiji”

November 21, 2025

MVUA ILIYONYESHA LUMBILA IWAMBI MBEYA MITARO YAFURIKA MAKAZI YA WATU YAJAA MAJI BIASHARA ZASIMAMA

November 21, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Mbinu ya kupata faida katika biashara ya samaki, uvuvi

November 21, 2025

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE

November 21, 2025

Mgombea Umeya Jiji la Mbeya, Noah Mwakisu Arejesha Fomu; Aahidi “Ukombozi wa Jiji”

November 21, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025228

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.